Oranje (mto)

(Elekezwa kutoka Mto Oranje)

Oranje (kwa Kiingereza Orange River) ni mto mrefu wa Afrika Kusini.

Mto wa Oranje
Maporomoko ya Augrabies ya Mto Oranje karibu na Upington
Chanzo Milima ya Maloti (Drakensberg) nchini Lesotho
Mdomo Atlantiki mpakani pa Namibia na Afrika Kusini
Nchi Lesotho, Afrika Kusini, Namibia
Urefu 2,160 km
Kimo cha chanzo 1,600 m
Mkondo 800 m³/s
Eneo la beseni 941,421 km²

Chanzo chake ni katika milima ya Maloti (Drakensberg) nchini Lesotho. Mdomo uko Atlantiki mpakani kati ya Afrika Kusini na Namibia.

Pale inapokaribia mpaka wa Nambibia Oranje imechimba mfereji mrefu katika miamba ina maporomoko yake makubwa ya Augrabies. Kwa 500 km mwendo wa mto ni mpaka kati ya Afrika Kusini na Namibia. Mjini Oranjemund Oranje inaingia bahari ya Atlantiki.

Njiani Oranje inabeba kiasi kikubwa cha mashapo hasa mchanga hadi baharini. Hapa husukumwa kusini na mkondo wa baharini ya Benguela. Mchanga huu ni sehemu kubwa ya mchanga wa jangwa la Namib na matuta makubwa ya mchanga yanayopatikana kwenye pwani ya Namibia.

Pinde la mto Oranje wakati wa mvua

Jina la Oranje ni Kiafrikaans (pia Kiholanzi) limetokana na familia ya wafalme wa Uholanzi. Neno lamaanisha rangi ya machungwa mabivu.

Kwa ujumla Oranje hailishi mimea mengi njiani yake inapopita katika nchi yabisi. Lakini kuna sehemu mbalimbali ambako maji yake huchukuliwa na mitambo kumwagilia mashamba.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Oranje (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.