Nathan Söderblom
Lars Olof Jonathan Söderblom (15 Januari 1866 – 12 Julai 1931) alikuwa askofu wa Kanisa la Kilutheri kutoka nchi ya Uswidi. Hasa alijitahidi upande wa umoja wa madhehebu. Mwaka wa 1930 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
Maisha
haririSöderblom alizaliwa kijijini katika eneo la Söderhamn, Uswidi. Baba yake alikuwa mchungaji mwenye imani imara.
Mwaka wa 1883, Söderblom aliingia chuo kikuu cha Uppsala. Alimfuata baba yake katika masomo ya teolojia na kuwekwa wakfu kama mchungaji mwaka wa 1893.
Mwaka wa 1912 aliteuliwa kuwa profesa wa masomo ya dini katika chuo kikuu cha Leipzig, Ujerumani. Baada ya miaka miwili tu ilimbidi kurudi Uswidi kwa vile aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri nchini kwake. Kama kiongozi wa kanisa, alijitahidi hasa kwa ajili ya umoja wa madhehebu, na alikuwa rafiki wa karibu wa George Bell, mchungaji Mwingereza.
Viungo vya nje
hariri
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nathan Söderblom kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |