Ncha ya kijiografia

(Elekezwa kutoka Ncha za kijiografia)

Ncha ya kijiografia ni moja kati ya mahali pawili ambapo mhimili wa mzunguko wa dunia unakutana na uso wa dunia. Kwa maana hiyohiyo ncha zinapatikana pia kwenye sayari, mwezi au gimba la angani kubwa lingine linalozunguka kwenye mhimili wake.

Dunia inazunguka kwenye mhimili wake unaoonyeshwa na mstari mweupe. Ncha iko mahali ambako mstari huo unapita uso wa dunia. Picha hii inatazama dunia upande, hivyo ni ncha ya kaskazini pekee inayoonekana.

Ncha mbili kwa kawaida hutofautishwa kwa kuziita "ncha ya kaskazini" na "ncha ya kusini" jinsi ilivyo kwenye dunia yetu. Kila ncha iko nyuzi 90 kutoka mstari wa ikweta.

Kwenye magimba ya angani kama dunia yetu mara kwa mara kuna mabadiliko madogo ya mzunguko yanayosababisha ncha kuhama kiasi. Kwa sababu hiyo mahali kamili pa ncha za dunia huhama mita chache kila mwaka. Ramani na data za kijiografia hutumia wastani kati ya mahali pa namna hiyo.

Kama gimba la angani lina uga sumaku kuna pia ncha sumaku. Kwa dunia yetu mhimili wa uga sumaku uko karibu na mhimili wa mzunguko na kwa hiyo ncha sumaku na ncha ya jiografia ziko tofauti lakini karibu. Lakini si lazima iwe hivyo kwa kila sayari. Kwenye sayari ya Uranus kuna tofauti wa nyuzi 60.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.