Ndegeputo
Ndegeputo (au purutangi) ni chomboanga kinachoelea kwa nguvu elezi ya gesi iliyoko ndani ya ganda lake. Chini ya chumba cha gesi inabeba behewa ya abiria na mizigo. Inasukumwa na injini za parapela.
Kimsingi kuna aina mbili za ndegeputo:
Ndegeputo isiyo na fremu ("Blimp")
haririKimsingi aina hii ni fuko kubwa lenye gesi nyepesi (heli) ndani yake linalobeba behewa chini yake. Injini zafungwa kwenye behewa. Faida yao ni ya kwamba ni rahisi kuzisafirisha kwenye nchi kavu baada ya kuondoa gesi ndani yake. Fuko hukunjwa na haichukui nafasi kubwa. Bei si kubwa sana. Hasara ni ya kwamba haiwezekani kuongeza kukubwa juu ya kiwango fulani. Blimpu kubwa zinazopatikana hubeba hadi watu 10 au mzigo unaolingana.
Zapendwa sana kwa shughuli za matangazo ya kibiashara pia kwa safari za kitalii.
Ndegeputo yenye fremu ya ndani
haririKwa vyomboanga vikubwa zaidi ndegeputo zilipewa fremu ya ndani. Fremi hii yawezesha kufungwa kwa injini sehemu mbalimbali za chombo kinachoboresha uwezo wake wa kulengwa.
Kmapuni ya kwanza iliyoboresha muundo huo ilikuwa Zeppelin ya Ujerumani tangu mwaka 1900. Usafiri wa mbali angani ulifanywa hasa kwa Zeppelin hadi maafa ya Lakehurst mwaka 1937. Ndegeputo kubwa kabisa ilichomwa moto kwa sababu ilijazwa gesi ya hidrojeni ilishikwa na moto.
Ndegeputo za baadaye zilijazwa heli ambayo ni gesi nyepesi yenye uwezo mdogo wa nguvu elezi kuliko hidrojeni lakini haishiki moto.
Lakini usafiri wa abiria ulikwama baada ya maafa ya 1937 halafu ulipitiwa na maendeleo ya ndege.
Leo hii kampuni ya Zeppelin imeanza tena kujenga ndegeputo kwa mfumo ulioboreshwa wa "NT" ("neue Technologie/new technology" - teknolojia mpya) .
Huduma za kwanza za usafiri wa angani zilitekelezwa na ndegeputo. Tangu vita kuu ya kwanza ya dunia ndege ziliendelea zikaonekana ya kwamba zilikuwa usafiri wa haraka zaidi lakini hazikufika mbali bado. Ndege zilihitaji kushuka na kuongeza petroli kila baada ya masaa kadhaa lakini ndegeputo kubwa ziliweza kukaa hewani kwa siku mfululizo. Kabla ya vita kuu ya pili ya dunia ndegeputo za Zeppelin zilikuwa vyomboanga vya pekee vilivyosafirisha abiria mara kwa kati ya Ulaya na nchi za Amerika.
Maendeleo ya ndege wakati wa vita kuu ya pili ya dunia na baadaye imeondoa ndegeputo katika usafiri wa kawaida. Ndege hubeba abiria na mizigo haraka zaidi, hubeba mizigo mikubwa zaidi tena katika kila hali ya hewa wakati ndegeputo zina matatizo kama upepo ni mkali mno au halijoto yapanda mno inayosababisha gesi ndani ya ganda kuenea sana.
Matumizi ya ndegeputo leo
haririSiku hizi ndegeputo zatumiwa hasa kwa shughuli tatu:
- fuko la gesi latumiwa kwa matangazo ya kibiashara. Ni hasa blimp ndogo zinazokodishwa kuonyesha matangazo haya juu ya miji mikubwa au penye mikutano ya watu wengi.
- kwa safari za kitalii kwa muda mfupi ndegeputo ina faida ya kutembea polepole kwenye kimo kidogo hali inayowezesha abiria kutazama vizuro yote yaliyopo chini yao.
- kwa utafiti wa kisayansi na shughuli za usimamizi; uwezo wa kulea polepole kwa kimo kidogo tena kwa muda mrefu wawezesha vipimo vya kisayansi kufanyiwa kwa makini kushinda vipimo kwa njia za ndege.
- Faida hii yatumiwa pia kibiashara. Zeppelin NT mpya imekodiwa na kampuni De Beer ya Afrika Kusini tangu 2005 kwa vipimo vya kutafuta almasi katika Botswana na inasemekana kwa matokeo bora kushinda vipimo vya awali kwa ndege au helikopta.
- Ndegeputo zatumiwa kwa usimamizi wa mikutano mikubwa kwa mfano michezo ya Olimpiki ya Athens ya 2004 au mkutano wa vijana wa dunia wa kanisa katoliki huko Köln mwaka 2006.