Nerei ni Mkristo wa Roma ya Kale anayeheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini pamoja na Achilei.

Watakatifu Nerei, Achilei na Domitila walivyochorwa na Peter Paul Rubens.

Habari zao zimesimuliwa na Papa Damaso I; kwamba walikuwa wamejiunga na jeshi, na kwa hofu walikuwa tayari kutii amri mbovu za hakimu, lakini kwa kumuongokea Mungu wa kweli, walitupilia mbali ngao, mavazi ya kijeshi na mikuki, waliacha kambi na kwa kukiri imani yao kwa Kristo, waliuawa.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Mei[1][2], siku ambayo maiti zao walizikwa katika makaburi ya Domitila mjini Roma.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana), p. 123
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.