Ngao (kwa Kilatini na Kiingereza Scutum - Shield) [1] ni jina la kundinyota dogo kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia yetu.

Nyota za kundinyota Ngao (Scutum ) katika sehemu yao ya angani

Mahali pake hariri

Ngao lipo angani kati ya makundinyota ya Kausi (Mshale) (Sagittarius) na Ukabu (Aquila) likigusana pia na Hayya (Serpens). Lipoo karibu na ikweta ya anga.

Jina hariri

Kundinyota hili halikujulikana kwa mabaharia Waswahili wa Kale wala kwa Waarabu au Wagiriki kwa sababu nyota zake ni hafifu na chache. Nyota zake zilihesabiwa zamani pia kama sehemu ya kundinyota Ukabu. Scutum – Ngao Ilitajwa mara ya kwanza kama kundi la pekee na mwanaastronomia Johannes Hevelius kutoka Danzig (Ujerumani / Poland) . Hevelius aliyeandika kwa Kilatini alichagua jina “Scutum” na hapo alimaanisha ngao ya mfalme wa Poland akitaka kumheshimu baada ya mapigano ya Vienna ya mwaka 1683 ambako jeshi la Poland liliwashinda Waosmani na kuokoa mji mkuu wa Milki ya Ujerumani.

Hevelius akiwa mpika pombe na mfanyabiashara tajiri aliyeendelea kushika kwa muda pia uraisi wa mji wake alikuwa maarufu hasa kwa kuangalia, kupima na kuorodhesha nyota pamoja na mke wake Elisabeth Hevelius.

Scutum - Ngao lipo kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2] kwa jina la Scutum. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Sct'.[3]

Nyota hariri

Ngao –Scutum lina nyota chache tu. Nyota angavu zaidi ni Alfa Scuti yenye mag 3.85 ikiwa umbali wa miaka nuru 199 kutoka Dunia[4].

Tanbihi hariri

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Scutum " katika lugha ya Kilatini ni "Scuti" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Scuti, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  4. [ http://stars.astro.illinois.edu/sow/alphasct.html ALPHA SCT (Alpha Scuti)], tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngao (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.