Nicolas Pépé

Mchezaji wa soka wa Ivory Coast

Nicolas Pépé (alizaliwa Mantes-la-Jolie, Ufaransa, 29 Mei 1995) ni mchezaji wa soka wa Ivory Coast ambaye anachezea katika klabu ya Arsenal ya Uingereza na timu ya taifa Ivory Coast.

Nicolas Pepe akiwa Lille.

Maisha hariri

Pépé alianza kazi yake kama golikipa wa Solitaire Paris hadi alipokuwa na miaka 14, baadae alibadili maamuzi na kucheza kama kiungo.

Angers hariri

Alitia saini katika klabu ya Angers mnamo 2013, na alitumia msimu wake mmoja tu. Alifanya mazoezi yake ya kwanza kwenye raundi ya pili ya Ligue 1 na upotezaji mechi ya kwanza tuwa nyumbani 2-1.

Lille hariri

Mnamo tarehe 21 Juni, 2017, Pépé alisaini mkataba wa miaka mitano na Lille, kwa ada ya uhamisho wa milioni 10, Mnamo tarehe 15 Septemba, 2018, wakati wa msimu wa 2018-19, Pépé alifunga mabao matatu katika ushindi wa nyumbani wa 3-2 dhidi ya Amiens. Siku kadhaa baadaye, ilithibitishwa na rais wa klabu Gérard Lopez kwamba FC Barcelona walikuwa kati ya vilabu kadhaa ambavyo vilikuwa na nia ya kumsaini.

Arsenal hariri

Mnamo tarehe 1 Agosti 2019, ilitangazwa kuwa Pépé alijiunga na Klabu ya Uingereza Arsenal katika ada ya milioni 78), akilinganisha rekodi ya awali ya milioni 62 ya Pierre-Emerick Aubameyang, alikabidhiwa jezi namba 19 mgongoni.

Pépé anajulikana kama mshambuliaji mwenye kasi na mwenye ujuzi wa kushambulia ambaye yuko vizuri pande zote mbili, lakini kawaida hucheza upande wa kulia akitumia mguu wake wa kushoto, kabla alikuwa akicheza kama kiungo lakini alibadilishwa na meneja wa Lille OSC Marcelo Bielsa kucheza kama mshambuliaji.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nicolas Pépé kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.