Nidhamu (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "discipline") ni adabu njema kwenye familia, jeshi, hata kwenye shule. Mtu mwenye nidhamu ni mtu ambaye anafanya kinachotakiwa kufanywa ili kufikia malengo yake na ya jamii.

Kuwa na mawazo mazuri tu kunadai juhudi. Hilo ni lengo mojawapo la nidhamu.

Kufanya mtoto kuwa na nidhamu pengine ni kwa kumuadhibu pindi anapoonesha tabia mbaya. Kuchapa kulichukuliwa kama aina ya nidhamu.

Hata hivyo muhimu zaidi ni nidhamu binafsi, ambayo ni kujitawala kwa kusimamia matendo na hata mawazo yako mwenyewe yawe ya kufa tu.

Nidhamu ya kijeshi inafundisha watu kuheshimu sheria na amri. Mwanajeshi mwenye nidhamu ni mtu ambaye anaweza kutenda hata akiogopa kwa maisha yake.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nidhamu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.