Uzima wa milele

Uzima wa milele ni hali ya kuishi bila mwisho.[2]

Fountain of Eternal Life huko Cleveland, Ohio, Marekani. Inamaanisha "Binadamu kuinuka juu ya kifo, akimuelekea Mungu na Amani".[1]

Biolojia inaonyesha kuwa uhai wa mwili una mipaka, wala sayansi na teknolojia hazijaweza kuivuka.

Hata hivyo, toka zamani binadamu ameonyesha kwa njia nyingi hamu ya kuendelea kuishi kwa namna moja au nyingine.

Utenzi wa Gilgamesh, kimoja kati ya vitabu vya kwanza vya fasihi andishi (karne ya 22 KK hivi), kinasimulia habari za mtu aliyetaka kuishi milele.[3]

Katika dini

Katika dini mbalimbali, uzima wa milele unatarajiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (au miungu) kama tuzo kwa matu aliyefuata uadilifu wakati wa kuishi duniani.

Uzima wa milele ndio ahadi kuu ya Yesu kwa wafuasi wake, hasa kadiri ya Injili ya Yohane. Sura ya 17 ya Injili hiyo inafafanua uzima wa milele kuwa uhusiano na Mungu na Yesu Kristo mwenyewe.

Kwa ahadi hiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake. “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3). “Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet 1:3-4). Sisi tuliobatizwa tunaitwa “wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!” (1Yoh 3:1). Kwa sababu tumesadiki kwamba “Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8) na kwamba “hakuna lisilowezekana kwa Bwana” (Lk 1:37). “Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ‘Aba!’ yaani, ‘Baba!’ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu” (Gal 4:6-7).

Tanbihi

  1. Marshall Fredericks (2003). GCVM History and Mission. Greater Cleveland Veteran's Memorial, Inc.. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-02-16. Iliwekwa mnamo 2009-01-14.
  2. Oxford English Dictionary "Immortality"
  3. Joel Garreau (October 31, 2007). "The Invincible Man". The Washington Post: C01. http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2007/10/30/AR2007103002222_pf.html.

Marejeo

Viungo vya nje

Mtazamo wa kidini na wa kiroho

Katika fasihi

  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uzima wa milele kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.