Ntobo (Msalala)
(Elekezwa kutoka Ntobo (Kahama))
Kwa kata nyingine yenye jina hili, tazama Ntobo (Igunga).
Ntobo ni kata ya Wilaya ya Msalala katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania. Ntobo ni makao makuu mapya ya Halmashauri mpya ya Msalala wilayani Kahama.
Kata hiyo ina vijiji vitano ambavyo ni: Ntobo A, Ntobo B, Bukwangu, Kalagwa, na Buganzo.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,224 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,089 waishio humo.[2]
Shughuli kubwa ya kiuchumi kwa wakazi wa kata hiyo ni kilimo.
Marejeo
haririKata za Wilaya ya Msalala - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bugarama | Bulige | Bulyan'hulu | Busangi | Chela | Ikinda | Isaka | Jana | Kashishi | Lunguya | Mega | Mwakata | Mwalugulu | Mwanase | Ngaya | Ntobo | Segese | Shilela
|