Ngaya ni kata ya Wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Msalala katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania. Kata hiyo imepakana na kata za Chela, Busangi, Bulige, Nduku na Mhongolo.

Ina vijiji sita navyo ni Butegwa, Kakulu, Mhama, Mwashimbai, Ngaya na Igombe.

Wakazi

hariri

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 16,599 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,681 waishio humo.[2]

Wakazi wa eneo hili ni Wasukuma, Wadakama na Wanyamwezi, pia wamechanganyikana sana na kwa sasa ni vigumu kuwatenganisha.

Wakazi wa eneo hili wanajishughulisha na kilimo na biashara. Kilimo kikuu ni mpunga na mahindi; mazao mengine katika kata hii ni pamoja na viazi vitamu, karanga, maharage, mbaazi na njugu mawe.

Shughuli kuu za biashara ni biashara ya wanyama wakiwemo ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku. Minada ya biashara kwa wakazi hawa ni mnada wa Nduku, wa Burige, wa Mwakitolyo, wa Masabi; wengine husafiri mpaka Salawe, Manzese (Busoka) na Bukombe.

Biashara ya mazao, kama vile mahindi, mpunga, viazi vilivyokatwa, mihogo na karanga hufanyika kwa siku maalumu kwa kila kata zinazozunguka kata hiyo: masoko hayo hupatikana Busangi, Ngaya, Chela, Bulige, Nduku na mjini Kahama, mengine ni Segese, Ntobo na Nundu.

Maeneo ya kihistoria

hariri

Ngaya ni moja kati ya himaya za kitemi zilizokuwepo hapo kale kabla ya ujio wa wakoloni.

Kuna:

Maeneo mengine ya vivutio ni mto Ngaya, unaomwaga maji yake katika ziwa Viktoria, pia mashamba makubwa ya mipunga katika vijiji vya Mwashimbai, Kakulu, Mhama na Igombe.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Msalala - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania  

Bugarama | Bulige | Bulyan'hulu | Busangi | Chela | Ikinda | Isaka | Jana | Kashishi | Lunguya | Mega | Mwakata | Mwalugulu | Mwanase | Ngaya | Ntobo | Segese | Shilela

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ngaya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.