Nyoka-maji
Nyoka-maji kahawia (Lycodonomorphus rufulus)
Nyoka-maji kahawia (Lycodonomorphus rufulus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Lamprophiinae (Nyoka wanaofanana na chata)
Fitzinger, 1843
Jenasi: Lycodonomorphus
Lichtenstein, 1823
Ngazi za chini

Spishi 9:

Nyoka-maji ni nyoka wasio na sumu wa jenasi Lycodonomorphus katika familia Lamprophiidae. Kuna nyoka-maji katika jenasi Grayia wa familia hiyo hiyo pia, lakini nyoka hawa ni warefu zaidi mara mbili. Na pia tena kuna nyoka-maji katika familia Colubridae.

Spishi hizi ni fupi kiasi, sm 70 kwa kipeo lakini sm 35-60 kwa kawaida. zina mkia mfupi, kichwa kidogo na macho madogo. Rangi yao ni nyeusi, kijivu, kahawia, hudhurungi, kahawia-zeituni au kijani-zeituni juu na mara nyingi njano au machungwa chini.

Nyoka-maji huishi majini na hula vyura na samaki wadogo.

Nyoka hawa hawana sumu na kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila hatari.

Nyoka-nyumbani

hariri

Spishi moja, nyoka-nyumbani mweusi (Lycodonomorphus inornatus) ni tofauti na spishi nyingine za jenasi hii. Haiishi majini na inaweza kuingia nyumba. Hula mijusi, nyoka wengine na wagugunaji wadogo. Nyoka huyu ni mrefu kuliko wenzake, hadi sm 130.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-maji kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.