Nyoka-misitu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Oppel, 1811
Jenasi: Buhoma
Ziegler, Vences, Glaw & Böhme, 1997
Ngazi za chini

Spishi 3:

Nyoka-misitu ni nyoka wa jenasi Buhoma katika familia Lamprophiidae ambao wanatokea misituni kwa Afrika ya Magharibi na ya Mashariki. Kuna spishi nyingine ya nyoka-misitu katika jenasi Hormonotus, nyoka-misitu njano.

Nyoka hawa sio warefu sana, sm 52 kwa kipeo lakini sm 20-35 kwa kawaida. Rangi yao ni kahawia au kijivu na mara nyingi wana mlia au milia myeusi myembamba mgongoni. Tumbo ni kijivu, hudhurungi au maziwa.

Nyoka laini hukiakia mchana misituni na hupumzika chini ya magogo, matawi au majani makavu au katika vishimo. Hula vyura hasa.

Nyoka hawa wana sumu na kwa ajili ya ukubwa wao mdogo hawawezi kung'ata watu na hawashambulii. Lakini wakiokotwa hutoa kinyaa kinukacho kutoka kloaka.

Spishi hariri

Marejeo hariri

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-misitu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.