Nyuki-bungu mdogo
Nyuki-bungu mdogo | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ceratina bifida
| ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||||
Makabila 3, jenasi 16:
|
Nyuki-bungu wadogo au bungu wadogo ni nyuki wadogo wa makabila Allodapini, Ceratinini na Manueliini katika nusufamilia Xylocopinae wa family Apidae wanaojenga viota vyao ndani ya ubao uliooza au katika vitawi, mashina au mabua yenye moyomti mwororo. Spishi kadhaa huonyesha viwango mbalimbali vya kuwa na viota katika jamii, lakini hakuna hata mmoja wao ambaye ni ya kijamii kama nyuki-asali. Wanatokea katika mabara yote isipokuwa Antakitiki.
Spishi za kabila Xylocopini huitwa nyuki-bungu wakubwa.
Maelezo
haririNyuki hawa hutofautiana kwa ukubwa kutoka mm 4 hadi 16. Wao ni wembamba na hawana mwili imara kama nyuki-bungu wakubwa. Wanaweza kuwa weusi,kijani au buluu, mara nyingi na mng'ao wa metali. Kunaweza kuwa na nyekundu kwenye fumbatio au njano kwenye sehemu kadhaa za mwili. Nywele kwenye mwili ni fupi na siyo nyingi, ingawa baadhi ya spishi katika Allodapini wana thoraksi yenye nywele ndefu kiasi. Kuna skopa isiyo imekua sana ya nywele ndefu zaidi kwenye tibia inayotumika kushikilia chavua iliyokusanywa.
Nyuki wa jenasi Manuelia huwa wapweke, lakini majike huvumilia zaidi majike wengine katika koloni moja la viota kuliko majike kutoka makoloni mengine. Hii inachukuliwa kuwa hatua ya kwanza katika mageuko ya ujamii. Jenasi Ceratina ina spishi mpweke na za ujamii dhaifu, huku spishi za kabila Allodapini zote zinaonyesha viwango tofauti vya ujamii. Nyuki-bungu wadogo huchimba ndani ya ubao unaooza au vitawi au mashina yenye kiini au moyomti mwororo. Baadhi ya spishi huunda vijumba vya kizazi, kila moja ikiwa na donge la chavua na mbochi ambayo jana mmoja hula. Spishi nyingine hazitengenezi vijumba vya kizazi bali hutaga mayai kwa safu ndani ya handaki la kiota. Majana yao hulishwa kila siku na kioevu kilichorudishwa kutoka kwa gole.
Nyuki-bungu wadogo wengi ni wachavushaji muhimu wa aina nyingi za maua.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri
|
|
|
Picha
hariri-
Allodapula variegata
-
Ceratina moerenhouti
-
Kiota cha Ceratina sp. katika bua la shamari