Open main menu
Mti wa uhai huonyesha mabadiliko wa spishi tangu mwanzo wa uhai

Mageuko ya spishi (ing. evolution) ni nadharia ya kisayansi iliyobuniwa na kutumiwa na wataalamu wa biolojia, hasa tawi la jenetikia.

Inasema ya kwamba spishi za viumbehai zilizopo duniani leo zimetokana na spishi zilizokuwa tofauti za zamani.

Nadharia hii inategemea hoja ya kwamba awali uhai wote ulitokana na maumbo asilia.

Katika wazo hili spishi zote jinsi zilivyo sasa zinaendelea kubadilika.

Msingi wa nadharia hii ni mabaki ya kisukuku ya viumbehai ambao hawapo tena duniani lakini wanafanana kiasi na viumbehai wa leo, pamoja na ulinganifu wa spishi za karibu na za mbali zaidi. Nadharia ya mageuko ya spishi inalenga kueleza mabadiliko hayo.

Leo hii ndiyo nadharia ya kibiolojia inayokubaliwa na wataalamu wengi hata kama kuna wapinzani kadhaa, hasa upande wa wenye imani kali ya dini, lakini pia wachache kwa sababu za kitaalamu.

Mchango wa DarwinEdit

Mtaalamu Mwingereza Charles Darwin anajulikana kama mvumbuzi wa nadharia hii.

Kadiri yake, mageuko hayo hufuata uteuzi asilia yaani viumbehai wanaolingana vizuri zaidi na mazingira wanaishi na kuzaa kushinda viumbehai wasiolingana nayo.

Kwa njia hiyo tabia za viumbehai wanaofaa zaidi zinazidi kuendelezwa kwa sababu watoto wao hurithi tabia hizo. Lakini tabia za viumbehai wasiofaa sana zinaweza kutoweka kwa sababu wanakufa mapema na hawana watoto wengi wanaoendeleza tabia zao.

Darwin alishambuliwa mara nyingi kwa hoja ya kwamba mafundisho yake yanapinga taarifa ya uumbaji katika Biblia. Lakini hiyo inategemea jinsi masimulizi yake yanavyosomwa: si lazima mwamini achukue kila kitu kama ilivyoandikwa, kwa sababu Biblia hailengi kutufundisha sayansi, bali njia ya wokovu.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu: