Nyumba ya Wawakilishi ya Marekani
Nyumba ya Wawakilishi ya Marekani (kwa Kiingereza: United States House of Representatives) ni sehemu ya bunge la Marekani (US Congress) linaloamua kuhusu sheria za Muungano wa Madola ya Amerika. Tawi lingine la Bunge ni Senati ya Marekani. Kuna jumla ya wabunge 435 katika Nyumba ya Wawakilishi.
Idadi ya wawakilishi kutoka kila mojawapo kati ya majimbo ya Marekani, ambayo ni 50, hutegemea idadi ya wakazi katika jimbo hilo, lakini kuna mwakilishi angalau mmoja kwa kila jimbo.
Kila baada miaka 10, kuna sensa ya kitaifa na ugawaji wa idadi ya wawakilishi huangaliwa upya baada ya sensa kwa kupunguza au kuongeza idadi kwa majimbo husika kulingana na hesabu hiyo.
Wawakilishi hukutana ndani ya jengo la Capitol mjini Washington, DC.
Mwenyekiti wa Nyumba ya Wawakilishi ana cheo cha spika, na spika kwenye mwaka 2020 ni Nancy Pelosi.
Kulingana na Katiba ya Marekani, sheria zote zinazohusu mapato na matumizi ya serikali zinaanza kujadiliwa katika Nyumba ya Wawakilishi.
Wawakilishi wana pia mamlaka ya kufungua mashtaka dhidi ya maafisa wa kitaifa kama vile rais au majaji wa mahakama kuu.
Nyumba kwa sasa ina wawakilishi kutoka Chama cha Kidemokrasia cha Marekani (Democratic Party) 233, Chama cha Jamhuri cha Marekani (Republican Party) 196, Chama cha Libertarian 1 na wabunge 5 wasioshikamana na chama chochote.
Tovuti nyingine
hariri- Tovuti rasmi
- Legislative information and archives for US House and Senate, via Congress.gov
- Biographical Directory of the United States Congress, 1774 to Present
- A New Nation Votes: American Election Returns 1787–1825 Archived 25 Julai 2008 at the Wayback Machine.
- Complete Downloadable List of U.S. Representative Contact Information, via AggData LLC]
- Information about U.S. Congressional Bills and Resolutions Archived 2 Januari 2020 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |