Nzi mweupe
Nzi mweupe wa kiazi kitamu (Bemisia tabaci)
Nzi mweupe wa kiazi kitamu (Bemisia tabaci)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Lang, 1888
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Sternorrhyncha
Familia ya juu: Aleyrodoidea
Familia: Aleyrodidae
Westwood, 1840
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:

Nzi weupe ni wadudu wadogo wa familia Aleyrodidae katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wadudu hawa wanaweza kuwa wasumbufu kama vidukari, hususa wakiwa tele, kwa sababu wanafyunza utomvu pia na kuvu nyeusi inakua juu ya mana wanayochoza na inayoanguka kwenye majani. Kuvu hii inazuia majani yasifanye usanidimwanga na mmea unanywea. Lakini hasara kubwa zaidi inayosababishwa na nzi weupe ni uwezo wao wa kusambaza magonjwa ya virusi za mimea. Kwa mfano, nzi mweupe wa kiazi kitamu anaweza kusambaza zaidi ya spishi kumi za virusi: virusi ya mosaiki ya mhogo ya Afrika (ACMV), virusi ya mosaiki ya dhahabu ya mharagwe, virusi ya mkunjo njano ya mnyanya (TYLCV) n.k. Nzi weupe wana adui wao kama wadudu-kibibi, wadudu mabawa-vena, wadudu-maua, nyigu wa kidusia n.k. Pia kuna kuvu viuawadudu (entomopathogenic fungi) inayoambukiza lava wa nzi weupe, kama Beauveria bassiana, Isaria fumosorosea na Metarhizium anisopliae.

Nzi weupe ni wadudu wadogo. Wapevu wa takriban spishi zote wana urefu wa mm 1-3, lakini spishi chache zinaweza kufika mm 5. Kiwiliwili cha nzi weupe kimerefuka kidogo na kinabeba mabawa manne ya ukubwa sawa ambayo yamepakiwa nta. Nta hii inawapatia rangi ya nyeupe. Vipande vya mdomo vimeungana katika mrija utumikao ili kufyunza utomvu. Hatua zote za nzi weupe (mayai, lava, wapevu) hupatikana kwa upande wa chini wa majani kwa kawaida.

Spishi zilizochaguliwa

hariri
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nzi mweupe kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.