Operesheni Magogoni
(Elekezwa kutoka Oparesheni magogoni)
Operesheni Magogoni ni jina la jitihada za kumficha rais wa Tanganyika, Julius Nyerere wakati wa uasi wa jeshi la Tanganyika Rifles kwenye mwezi wa Januari 1964.
Operesheni hiyo ilifanyika mapema asubuhi wa tarehe 20 Januari 1964 wakati wanajeshi kutoka katika kambi ya Colito Barracks,[1] walielekea ikulu ya Tanganyika ili kupeleka malalamiko na madai yao kwa rais.
Wakati wanajeshi walipofika ikulu, Nyerere hakuwepo, hivyo walinzi wake walioongozwa na Peter Bwimbo waliamua kutomrudisha ikulu bali kumtunza sehemu ya usalama.
Nyerere alisafirishwa na walinzi wake kwenda Kigamboni, na kufichwa katika eneo la Magogoni katika nyumba ya Mkristo.
Tanbihi
hariri- ↑ "MIAKA 20 BILA NYERERE: Nyerere apata msukosuko-5". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-02-02.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Operesheni Magogoni kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |