Kambi ya jeshi Lugalo

(Elekezwa kutoka Colito Barracks)

Kambi ya jeshi Lugalo ni kambi kubwa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania iliyoko jijini Dar es Salaam kwenye barabara ya Bagamoyo.

Ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Uingereza kama kambi ya King's African Rifles.

Ilipewa jina la "Colito Barracks" baada ya ushindi wa kikosi kutoka Tanganyika juu ya Waitalia katika mapigano ya Alaba Kulito huko Ethiopia tarehe 19 Mei 1941, wakati wa Vita Kuu ya Pili[1].

Uasi wa jeshi la Tanganyika Rifles wa mwaka 1964 ulianza hapo kwa njia ya mgomo wa wanajeshi.

Baada ya uhuru jina la kambi lilibadilishwa ili kukumbuka ushindi wa Wahehe chini ya mtemi Mkwawa juu ya jeshi la Kijerumani la Schutztruppe huko Lugalo uliotokea tarehe 17 Agosti 1891.

Ndani ya kambi iko Hospitali ya Lugalo ambayo ni hospitali ya rufaa kwa huduma za afya kwenye jeshi la Tanzania.

Marejeo

hariri
  1. "Kuhusu sajenti Leakey aliyekufa siku ile katika mapigano". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-06. Iliwekwa mnamo 2020-02-04.