Kwale (ndege)

(Elekezwa kutoka Ortygornis)

Kwa maana nyingine ya jina hili angalia hapa

Kwale
Kwale miguu-njano (Peliperdix coqui)
Kwale miguu-njano (Peliperdix coqui)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Galliformes (Ndege kama kuku)
Familia: Phasianidae (Ndege walio na mnasaba na kwale)
Horsfield, 1821
Nusufamilia: Perdicinae (Ndege wanaofanana na sikipi)
Horsfield, 1821
Ngazi za chini

Jenasi 6 za kwale:

Kwale (pia kware) ni ndege wa jenasi mbalimbali katika nusufamilia Perdicinae wa familia ya Phasianidae. Spishi za jenasi Pternistis zinatambuliwa kuwa na nasaba mbali kidogo na jenasi nyingine. Ingawa watu wengi huwaita kwale, sasa jina kereng'ende linapendelewa. Rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano. Hujificha kwa kawaida lakini sauti yao husikika mara kwa mara. Chakula chao ni mbegu, wadudu na nyungunyungu. Hutaga mayai matatu hadi kumi ardhini pengine juu ya manyasi makavu.

Karibu spishi zote zinatokea Afrika lakini spishi tano zinatokea Asia.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri