Oyani
Oyani wa Afrika ya Kati (Poiana richardsonii)
Oyani wa Afrika ya Kati (Poiana richardsonii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Viverridae (Wanyama walio na mnasaba na paka zabadi)
Nusufamilia: Viverrinae (Wanyama wanaofanana na paka zabadi)
Jenasi: Poiana
Gray, 1864
Ngazi za chini

Spishi 2:

Oyani (kutoka Kiing.: oyan[1][2]) ni wanyama mbua wadogo wa jenasi Poiana katika familia Viverridae. Wanafanana sana na linisang'i wa Asia (jenasi Prionodon) lakini wanyama hawa wana mnasaba zaidi na paka (Felidae) na wamo katika familia yao binafsi Prionodontidae[3]. Oyani wana mnasaba na kanu. Mfanano na linisang'i ni mfano wa mageuko ya ukaribiano.

Oyani ni wadogo (mwili wa sm 30 na mkia wa zaidi ya sm 30) lakini wembamba wenye miguu mifupi. Rangi yao ni aina ya njano na wana mabaka meusi (madoa, milia) na mkia una zingo nyeusi. Huishi mitini na hukiakia usiku. Hula vitu vyingu kama wanyama na ndege wadogo, wadudu, matunda, koko na machipukizi ya mimea.

Spishi hariri

Marejeo hariri

  1. Wozencraft, W. Christopher (2005). "Order Carnivora (pp. 532-628)". In Wilson, Don E., and Reeder, DeeAnn M., eds. Mammal Species of the World: A Taxonomic and Geographic Reference (3rd ed.). Baltimore: Johns Hopkins University Press, 2 vols. (2142 pp.). ISBN 978-0-8018-8221-0. OCLC 62265494
  2. Don E. Wilson , Russell A. Mittermeier (editors): Handbook of the Mammals of the World. Lynx Editions, Barcelona, 2009. ISBN 978-84-96553-49-1
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-01-25. Iliwekwa mnamo 2011-11-21.
  Makala hii kuhusu "Oyani" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili oyan kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni oyani.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.