Pankrasi wa Taormina
Pankrasi wa Taormina (Adana, leo nchini Uturuki, karne ya 1 - Taormina, Sicilia, Italia, 98 hivi) alikuwa Mkristo wa karne ya 1.
Inasemekana akiwa mtoto alimfahamu Yesu akabatizwa na Mtume Petro ambaye alimtuma Taormina kama askofu wa kwanza wa mji huo.
Baada ya kuongoa wengi, aliuawa kwa sababu ya imani yake[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Hieromartyr Pancratius the Bishop of Taormina in Sicily Orthodox Icon and Synaxarion
- The Priestly-Martyr Pancratius from The Prologue from Ohrid
- San Pancrazio di Taormina
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |