Paul Makonda

bashite

Paul Makonda (alizaliwa 15 Februari 1982) ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Tanzania.

Paul Makonda.

Alipata umaarufu wakati wa kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambapo alikuwa miongoni mwa wanachama wachache wa kikao maalumu cha bunge, waliotumwa kuandaa rasimu ya Katiba mpya.

Baadaye alipata umaarufu zaidi katika siasa za Tanzania, kwanza akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni halafu kama Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, John Pombe Magufuli[1] .

Makonda alikuwa mwanasiasa mwenye utata katika siasa za jiji, mara nyingi akikosoa upinzani, na kupiga vita vitendo vya ushoga na ukahaba jijini Dar es Salaam. Pia alikuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha taswira ya jiji na kupambana na umaskini.

Mnamo Januari 2020 Marekani ilitangaza kwamba Makonda na wanafamilia yake watapigwa marufuku kuingia Marekani kwa tuhuma ya kukandamiza haki za binadamu [2].

Mnamo 22 Oktoba 2023 halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilimteua kuwa katibu wa halmashauri kuu ya CCM taifa itikadi na uenezi[3].

Mnamo Aprili 2024 aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha baada ya John Mongela, aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, kuwepa majukumu mengine.

Marejeo

hariri
  1. https://www.bbc.com/swahili/habari-48701285
  2. https://www.reuters.com/article/us-usa-tanzania-sanctions/u-s-bans-tanzanian-official-who-launched-anti-gay-crackdown-idUSKBN1ZU2W9
  3. Edwin TZA (2023-10-22). "Paul Makonda ateuliwa Katibu wa CCM Taifa Itikadi na Uenezi". Millard Ayo (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-11-10.