Perpétue Nshimirimana
Perpétue Nshimirimana (alizaliwa Bujumbura, Februari 1961) ni mwanadiplomasia na mwandishi kutoka nchini Burundi.
Bi Nshimirimana alipata elimu ya juu ya secondari katika shule ya Lycée Clarté Notre Dame iliyopo katika mji Bujumbura kabla ya kusafiri hadi Algeria kwa ajili ya kujiunga na chuo kikuu, ambapo alipata diploma ya uandishi wa habari kutoka chuo cha National Institute for Media and Communication kilichopo nchini humo. Mnamo mwaka 1984 alirejea nyumbani Burundi na kupata nafasi ya kufanya kazi katika Radio na Televisheni ya taifa ya Burundi. Alihudumu kama mjumbe wa baraza la kitaifa la mawasiliano na tume ya kitaifa ya UNESCO. Kuanzia 1991 hadi 1992 alikuwa mjumbe wa tume ya katiba, na mnamo 1993 alihudumu katika tume ya kitaifa ya uchaguzi. Baada ya kuchaguliwa kwa Melchior Ndadaye kama rais, Nshimirimana aliteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Burundi katika Umoja wa Mataifa huko Geneva, jukumu ambalo lilimalizika kwa kuuawa kwa Ndadaye baadaye mwaka wa 1993.[1] Kuanzia mwaka 2015 mwanadiplomasia huyu alihamishia makazi yake Uswisi. Kutokana na mchango wake kwa jamii mnamo 2005 Mwanadiplomasia huyu alipokea tuzo ya "Mwamke mtumwa anayeajiri" kwa lugha ya kifarensa iliitwa"Femme exilée, Femme engage" kwa kazi yake na watoto yatima wa Burundi.[2]
Mwanadiplomasia huyu ambaye wasifu wake maarufu kwa kichwa cha habari kinachosomeka "barua kwa Isidore" ulichapishwa mnamo mwaka 2014.[1]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Perpétue Nshimirimana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |