Perth ni mji mkuu wa jimbo la Australia Magharibi uliopo kwenye kingo za Mto Swan.

Perth
Kitovu cha Jiji la Perth
Nchi Australia
Jimbo / Mkoa Australia Magharibi
Anwani ya kijiografia 31°57′8″S 115°51′32″E / 31.95222°S 115.85889°E / -31.95222; 115.85889
Kimo mita
Eneo km2 6,417.9
Wakazi 2,059,484 [1]
Msongamano wa watu 320.8969 / km2
Mahali km 3288 kutoka Sydney
Mahali pa Perth nchini Australia

Kuna wakazi karibu watu milioni 2.1 wanaoishi katika jiji hilo. [2] Ni mji mkubwa wa nne huko Australia, baada ya Sydney, Melbourne na Brisbane.

Perth ilianzishwa mnamo 1829 na nahodha James Stirling; huyu baharia alikuwa mwenyeji wa Uskoti hivyo alitumia jina la mji Perth wa Uskoti.

Perth ni maarufu kwa mchanga wake mweupe, mweupe. Fukwe zake ni bora kwa kuogelea. Kivutio maarufu cha watalii cha ndani ni Kisiwa cha Rottnest, ambacho kinakaliwa na wanyama wadogo wa kienyeji wanaoitwa Quokkas. Kivutio kingine maarufu ni Kings Park, ambayo ni mojawapo ya mbuga kubwa za jiji ulimwenguni.

Vyuo vikuu

hariri

Perth ina vyuo vikuu vifutavyo: [3]

  • Chuo Kikuu cha Australia Magharibi
  • Chuo Kikuu cha Murdoch
  • Chuo Kikuu cha Curtin
  • Chuo Kikuu cha Edith Cowan
  • Chuo Kikuu cha Notre Dame (Australia Magharibi) (kibinafsi)

Tabianchi

hariri

Tabianchi ni nusutropiki, kuna kipindi cha joto ambako hasa Januari na Februari hufikia viwango vya zaidi ya °C 31. Kinyume chake kuna miezi inayofanana na eneo la Mediteranea, katika miezi ya Juni hadi Agosti jotoridi hushuka chini °C 20 na kiasi cha mvua kinazidi milimita 120; jalidi (chini ya °C 0) hutokea mara chache. [4] [5] [6]

Marejeo

hariri
  1. "3218.0 – Regional Population Growth, Australia, 2017–18". Australian Bureau of Statistics. 27 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 22 Aprili 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) ERP at 30 June 2018.
  2. "Regional Population Growth, Australia 2008–2009". Australian Bureau of Statistics. 30 Machi 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Western Australian Universities Ilihifadhiwa 5 Septemba 2012 kwenye Wayback Machine. (accessed 2007-02-27)
  4. "Perth is Australia's windiest city | Did You Know That..?". didyouknowthat.org. 2011 [last update]. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-06. Iliwekwa mnamo August 31, 2011. {{cite web}}: Check date values in: |year= (help)
  5. "The Great Australian Weather Debate". gungahlinweather.com. 2008 [last update]. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-01. Iliwekwa mnamo August 31, 2011. officially be call {{cite web}}: Check date values in: |year= (help)
  6. "Did you know that...about Australia?". upfromaustralia.com. 2011 [last update]. Iliwekwa mnamo August 31, 2011. {{cite web}}: Check date values in: |year= (help)
  Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Perth kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.