Pierre Curie (15 Mei 1859 Paris/Ufaransa - 19 Aprili 1906) alikuwa mwanafizikia Mfaransa aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fizikia kwa mwaka 1903 pamoja na mke wake Marie Curie na Henri Becquerel.

Pierre Curie pamoja na Marie katika maabara.

Pamoja na mke wake alichunguza misingi ya sumakuumeme. Maelezo yao yaliunda misingi wa kuelewa unururifu wa kinyuklia.

Pierre Curie alishirikiana na mkewe Marie Curie pia katika ugunduzi wa elementi za poloni na radi hata baada ya kifo chake, mke akapata tuzo ya Nobel ya kemia.

Pierre Curie alikufa kutokana na ajali ya gari.

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pierre Curie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.