Marie Curie

Mwanafizikia na mkemia wa Kipolishi mwenye uraia wa Kifaransa (1867-1934)

Maria Curie (jina kamili: Maria Salomea Skłodowska-Curie; 7 Novemba 18674 Julai 1934) alikuwa mwanafizikia na mwanakemia Mpolandi na Mfaransa aliyepata Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka 1903 na Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka 1911. Marie Curie ni binadamu pekee aliyepokea tuzo ya Nobel kwa sayansi mbili tofauti.

Marie Curie mwaka 1900.

Maisha

hariri

Alizaliwa Poland kama Maria Skłodowska wakati nchi hiyo ilipokuwa chini ya Urusi. Wakati ule hapakuwa na nafasi kwa wanawake kusoma kwenye chuo kikuu nchini, hivyo akahamia Ufaransa mwaka 1891 akajiandikisha katika somo la fizikia akaendelea baadaye kuchukua digrii ya hisabati.

Mwaka 1895 akaolewa na mwanasayansi Mfaransa Pierre Curie. Pamoja naye alifanya utafiti wa unururifu akatambua elementi za poloni na radi.

Baadaye alikuwa profesa wa kike wa kwanza katika chuo kikuu cha Sorbonne mjini Paris.

Alikufa kutokana na kansa ya damu (lukemia) kwa sababu maishani mwake alishika dutu nururifu nyingi bila ya tahadhari wakati hatari za unururifu hazijajulikana.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marie Curie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.