Pinocchio (filamu ya 1940)
Pinocchio ni filamu ya katuni ya Marekani ya mwaka wa 1940 iliyotayarishwa na Walt Disney na inatokana na hadithi ya Kiitalia ya Carlo Collodi aliyesimulia vituko vya mwanaserere Pinokyo ("Le avventure di Pinocchio"). Kitabu hicho kiliwahi kutafsiriwa na Tanganyika Mission Press kwa Kiswahili mwaka 1965 na kuwa maarufu Afrika Mashariki kwa jina "Mambo yalioyompata Pinokyo".
Pinocchio | |
---|---|
Posta ya filamu | |
Imeongozwa na | Ben Sharpsteen Hamilton Luske Norman Ferguson T. Hee Wilfred Jackson Jack Kinney Bill Roberts |
Imetayarishwa na | Walt Disney |
Imetungwa na | Aurelius Battaglia William Cottrell Otto Englander Erdman Penner Joseph Sabo Ted Sears Webb Smith Based on the book by Carlo Collodi |
Nyota | Cliff Edwards Dickie Jones Christian Rub Mel Blanc Walter Catlett Charles Judels Evelyn Venable Frankie Darro |
Imesambazwa na | RKO Radio Pictures |
Imetolewa tar. | Februari 7, 1940 United States Februari 9, 1940 |
Ina muda wa dk. | 88 |
Nchi | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | US$2,289,247 |
Mapato yote ya filamu | $84,254,167[1] |
Hii ni filamu ya pili kutolewa katika mfululizo wa filamu za katuni za Walt Disney, na ilitengenezwa baada ya kupata mafanikio makubwa katika filamu ya awali ya Snow White and the Seven Dwarfs na ilitolewa katika makumbi na RKO Radio Pictures tarehe 7 Februari 1940.
Hadithi ya filamu hii inamhusisha kikaragosi cha mbao anayeitwa Pinocchio (sauti ya Dickie Jones) ameletwa maishani na kichimbakazi cha buluu (Evelyn Venable), ambaye anamweleza kwamba anaweza kuwa kijana wa kweli iwapo atajibitisha kama ni "jasiri, mkweli, na si mchoyo". Hivyo kikaragosi huyo anaianza safari ili ili awe kijana wa kweli, ambamo kunatokea mashambulizi mengi wakati wa safari hiyo.
Ndani yake wanakuja Aurelius Battaglia, William Cottrell, Otto Englander, Erdman Penner, Joseph Sabo, Ted Sears, na Webb Smith kutoka katika kitabu cha Collodi. Matayarisho yake yalisimamiwa na Ben Sharpsteen na Hamilton Luske, na mfululizo wa filamu uliongozwa na Norman Ferguson, T. Hee, Wilfred Jackson, Jack Kinney, na Bill Roberts.
Tazama pia
Marejeo
- ↑ "Pinocchio". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2009-06-10.
Viungo vya Nje
- (Kiingereza) Pinocchio katika Allmovie
- Pinocchio at the Big Cartoon DataBase
- Pinocchio katika Internet Movie Database
- Pinocchio katika Rotten Tomatoes