Sungura

(Elekezwa kutoka Pronolagus)
Sungura
Sungura wa Afrika (Lepus capensis)
Sungura wa Afrika (Lepus capensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Lagomorpha (Wanyama kama sungura)
Familia: Leporidae (Wanyama walio na mnasaba na sungura)
Fischer de Waldheim, 1817
Ngazi za chini

Jenasi 11:

Sungura ni wanyama wa jenasi mbalimbali katika familia Leporidae ambao wanaweza kukimbia kwa kasi sana. Sungura wa Ulaya (Lepus europaeus) anaweza kwenda hata mpaka km 72 kwa saa.

Huishi kwa upweke au kwa jozi, miili yao huweza kusharabu ya mvutano wa dunia wakati wa kukimbia, hivyo kuongeza kasi ya mbio.

Kwa kawaida mnyama huyu mwenye aibu, sungura wa Ulaya, hubadilika tabia yake wakati wa masika ambapo sungura hawa dume huonekana wakati wa mchana wakifukuzana. Hii huwa ni mashindano ya sungura dume kutawala eneo kubwa na hivyo huwa na jike wengi wakati wa msimu huu.

Sungura huonekana mpaka wakipigana kwelikweli. Kwa muda mrefu iliaminika kuwa mapigano haya yalikuwa baina ya dume wawili lakini sasa imefahamika kuwa baina ya jike na dume, labda huwa jike akikataa kujamiiana na wakati mwingine akimjaribu tu kama dume amejizatiti.

Sungura wanapatikana maeneo mengi sana na wameyazoea, na kuzaliana kwa haraka, hivyo hata uwindaji wao hauthaminiwi sana kama kwa wanyama wengine. Wakati fulani huko Amerika ya Kaskazini [1] walitumika sana kwa chakula, lakini kutokana na kiasi kidogo cha mafuta kwenye nyama zao hawatumuki kama chakula cha kutegemewa, [2] Sungura huandaliwa, huchomwa kama kawaida au kuliwa pamoja na mkate ama la.

Mtoto wa sungura huitwa kitungule.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri
  • Aztlanolagus agilis (Pliocene na Pleistocene za Marekani ya kusini na Mexiko ya Kaskazini)
  • Serengetilagus praecapensis (Miocene hadi Pleistocene ya Chad, Kenya, Maroko na Tanzania)

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.