Raffaele Rossi

Kardinali wa Italia wa Kanisa Katoliki la Roma

Raffaele Rossi, OCD, (28 Oktoba 1876 - 17 Septemba 1948) alikuwa Mkarmeli Peku kutoka Italia, halafu askofu na kardinali.

Raffaele Rossi

Rossi alihudumu katika Idara Takatifu ya Makardinali katika Curia ya Roma kuanzia mwaka 1930 hadi kifo chake.[1]

Akiingia shirikani, alichukua jina la kitawa Raffaele wa Mtakatifu Joseph. Papa Pius XI alimteua kuwa kardinali mwaka 1930.

Mchakato wa kumtangaza kuwa mtakatifu ulianza miongo mitatu baada ya kifo chake, na kwa sasa anajulikana kama Mtumishi wa Mungu.[2]

Rossi pia aliteuliwa kama mpelelezi wa stigmata za Padre Pio wa Pietrelcina kwa amri ya Papa Benedikto XV, na aliripoti kwake akieleza mtazamo mzuri kuhusu Mkapuchini huyo. Alitazama stigmata na kuzungumza na mtawa huyo huku akibainisha kwamba Padre Pio alikuwa "mkweli" na hakuwa na udanganyifu wala hila.

Marejeo

hariri
  1. Salvador Miranda. "Consistory of June 30, 1930 (XIII)". The Cardinals of the Holy Roman Church. Iliwekwa mnamo 27 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Servo di Dio Raffaele Carlo Rossi". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 27 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.