Wakarmeli (kwa Kilatini Ordo Fratrum Beatissimæ Virginis Mariæ de Monte Carmelo, kwa Kiingereza Order of the Brothers of the Blessed Virgin Mary of Mount Carmel, kifupi O.Carm.) ni watawa wa Kanisa Katoliki ambao labda ulianzishwa katika karne ya 12 kwenye mlima Karmeli (Israeli) ukizingatia juhudi za nabii Elia zilizojumlishwa katika maneno yake yanayotumika kama kaulimbiu ya shirika: "Zelo zelatus sum pro Domino Deo exercituum" (yaani "Nimefanya bidii sana kwa Bwana Mungu wa majeshi"). Pia kuna uhusiano wa pekee na Bikira Maria.

Nembo ya shirika.
Bikira Maria wa Mlima Karmeli na Wakarmeli watakatifu (Simon Stock (amesimama), Anjelo wa Yerusalemu (amepiga magoti), Maria Magdalena wa Pazzi, Teresa wa Yesu). Picha hii ya Pietro Novelli (1641) inatunzwa kwenye "Museo Diocesano", Palermo, Italia.
Sista mmonaki Mkarmeli akijisomea chumbani.

Mbali ya wanaume, wapo wanawake wamonaki wanaojifungia katika ugo wa monasteri, na masista wenye utume wa aina mbalimbali. Hatimaye wapo walei wanaofuata karama ya shirika ambayo ni hasa kuzama katika sala.

Walio wengi wanafuata urekebisho wa Wakarmeli Peku (kwa Kilatini "Ordo Carmelitarum Discalceatorum", kwa kifupi "O.C.D."), ulioanzishwa na Teresa wa Yesu katika karne ya 16 huko Hispania.

Watakatifu Wakarmeli

hariri

Wenye heri Wakarmeli

hariri

Marejeo

hariri
  • Schaff-Herzog Encyclopedia of Religion
  • Copsey, Richard and Fitzgerald-Lombard, Patrick (eds.), Carmel in Britain: studies on the early history of the Carmelite Order (1992–2004).
  • "The Carmelite Order" by Benedict Zimmerman. The Catholic Encyclopedia, 1908.
  • T. Brandsma, Carmelite Mysticism, Historical Sketches: 50th Anniversary Edition, (Darien, IL, 1986), ASIN B002HFBEZG
  • J. Boyce, Carmelite Liturgy and Spiritual Identity. The Choir Books of Kraków, Turnhout, 2009, Brepols Publishers, ISBN 978-2-503-51714-8
  • W. McGreal, At the Fountain of Elijah: The Carmelite Tradition, (Maryknoll, NY, 1999), ISBN 1-57075-292-3
  • J. Smet, The Carmelites: A History of the Brothers of Our Lady of Mt. Carmel, 4. vol. (Darien IL, 1975)
  • J. Welch, The Carmelite Way: An Ancient Path for Today’s Pilgrim, (New York: 1996), ISBN 0-8091-3652-X

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakarmeli kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.