Rayvanny

Mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania kutoka WCB Wasafi Record label


Raymond Shaban Mwakyusa (anafahamika zaidi kwa jina lake kama Rayvanny; amezaliwa 22 Agosti 1993) ni mwimbaji na mtunzi wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania (kwa asili ni mtu wa mkoani Mbeya).

Rayvanny
Jina la kuzaliwa Raymond Shaban Mwakyusa
Pia anajulikana kama Rayvanny
Amezaliwa 22 Agosti 1993 (1993-08-22) (umri 30)
Asili yake Mbeya,Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava,Afro Pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
Ala Piano, sauti
Miaka ya kazi 2011–mpaka sasa
Studio Wasafi Records,Next Level Music
Ame/Wameshirikiana na Harmonize, Diamond Platnumz
Tovuti Rayvanny

Wasifu

"Rayvanny" alianza kujulikana kupitia wimbo wake "Kwetu"[1] si siku nyingi sana tangu Harmonize atoe wimbo wake wa Bado.

Baadaye Natafuta Kiki, Sugu ambayo imetolewa kama wimbo wa ziada tu hasa ukizingatia umechukua biti ya Bow Wow (What's My Name). Halafu Mbeleko, Shikwambi, Zezeta na Kijuso aliyoimba na Queen Darleen, Pochi Nene aliyoimba na s2kizzy na baadaye Mwanza wimbo ambao aliimba na msanii mwenzie Diamond Platnumz. Wimbo huo ulifungiwa na Baraza la Sanaa nchini Tanzania BASATA kutokana na kutokuwa na maadili mema hivyo kufanya wimbo huo kufungiwa kupigwa kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania.

Baada ya wimbo huo kufungiwa yeye na Diamond walitoa wimbo uitwao Tetema, wimbo ambao ulipendwa na watu wengi kuufanya kuwa na watazamaji wengi kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mfupi sana.

Albamu

NYIMBO
Nambari Mada ya wimbo Mwaka Tan[2]
1. "Kwetu" 2016
2. "Natafuta Kiki" 2016
3. "Sugu" 2017
4. "Mbeleko" 2017
5. "Shikwambi" 2017
5. "Zezeta" 2017
6. "Chuma Ulete" 2017
7. "Unaibiwa" 2017
Nyimbo za kolabo
Nambari Mada ya Wimbo Mwaka Mwanamuziki mkuu Tan
1. "Salome" 2016 Diamond Platnumz
2. " Kijuso" 2017 Queen Darleen [3]
3. "Zilipendwa" 2017 Rich Mavoko, Diamond Platnumz, Mbosso, Harmonize, Lavalava, Queen Darleen [4][5][6]
1. "Cuppy jollof on the jet" 2020 Rema

Tanbihi

  1. "mtv news | top african acts to lookout for in 2017 | MTV Africa". www.mtvbase.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-15. Iliwekwa mnamo 2017-10-03.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  2. "You searched for RAYVANNY - Notjustok East Africa". Notjustok East Africa (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2017-10-03. 
  3. "VIDEO : Queen Darleen Ft. Rayvanny - Kijuso - Notjustok East Africa", Notjustok East Africa, 2017-02-20. (en-US) 
  4. "MTV News |wcb wasafi’s artists collaborate on "zilipendwa" | MTV Africa". www.mtvbase.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-18. Iliwekwa mnamo 2017-10-03.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  5. "Diamond Platnumz, Harmonize, Rich Mavoko, Rayvanny - Zilipendwa (Official Video) - AfroFire", AfroFire, 2017-08-26. (en-US) 
  6. "Rayvanny – Tetema (Remix) II Ft Patoranking, Zlatan & Diamond Platnumz - OlaGist", OlaGist, 2019-08-29. (en-US) 
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rayvanny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.