Yombeyombe

(Elekezwa kutoka Rhynchostruthus)
Yombeyombe
Yombeyombe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Ngazi za chini

Familia 3 na jenasi 8 zina yombeyombe (spishi 9 katika Afrika):

Yombeyombe au yombiyombi ni ndege wadogo wa familia mbalimbali. Spishi moja iko katika Ploceidae, moja katika Viduidae na 24 katika Fringillidae. Hawa ni ndege wanene yenye domo nene na rangi mbalimbali kama nyeusi, kahawia, njano na nyekundu kufuatana na spishi. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti au matete (yombeyombe wa kawaida). Hula mbegu lakini hulisha makinda yao wadudu. Yombeyombe wa kawaida hulifuma tago lake kwa majani ya manyasi katikati ya matete au mafunjo au pengine katika kichaka. Jike huyataga mayai 2-5. Yombeyombe wa Fringillidae hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika panda ya mti na jike huyataga mayai 2-7. Tofauti na yombeyombe wengine yombeyombe manjano hajengi tago lake mwenyewe lakini jike huyataga mayai katika matago ya spishi nyingine, k.m. spishi za videnenda na magamaga.

Spishi za Afrika

hariri

Familia Ploceidae

Familia Viduidae

Familia Fringillidae

Spishi za mabara mengine

hariri

Familia Fringillidae