Richelle Carey

Muandishi wa Habari wa Marekani

Richelle Carey (amezaliwa Houston, Texas, 13 Oktoba 1976) ni mwandishi wa habari na mrusha vipindi vya runinga wa nchini Marekani. Kwa sasa ni mhimili wa kipindi cha ‘’Al Jazeera English’’ na hapo awali alikuwa muendesha kipindi cha ‘’Al Jazeera America’’.

Hapo awali tena, Carey alikuwa msomaji wa taarifa za Habari wa televisheni ya ‘’HLN’’ na mwandishi wa Habari kuu za televisheni hiyo kuanzia May 2006 hadi Juni 2013 alijiunga na ‘’HLN’’ akitokea ‘’KMOV’’, St. Louis, Missouri. Kabla ya kujiunga na KMOV, wakati wa majira ya kiangazi ya mwaka 2003, Carey alikua msomaji wa taarifa ya Habari katika kituo cha ‘’Fox Broadcasting Company’’ yenye makazi yake huko Las Vegas, Nevada.

Carey alisoma katika chuo cha ‘’Smith College’’ huko Massachusetts lakini baadaye alihitimu katika chuo kikuu cha ‘’Baylor University’’ iliyopo Texas, ambamo alipata shahada ya mawasiliano.[1][2]

Kazi ya Utangazaji

hariri

Carey alianza safari ya utangazaji kwa kujitolea katika kituo ch televisheni cha ‘’KPRC-TV’’ jijini Houston, Texas. Baadaye alipandishwa cheo na kuwa msaidizi wa muandaaji vipindi katika kituo hicho hicho. Baada ya kuondoka KPRC, Carey alifanya kazi kama muandishi na mtangazaji wa Habari huko [Texas]], Nevada, na Missouri. Baadaye alihamia Atlanta kufanya kazi katika kituo cha HLN, ambapo alijikita zaidi katika kuwasemea wanawake na Watoto walioathiriwa na uovu. Wakati huo aliwahoji wanawake wengi walioshitakiwa kwa makosa mbalimbali. Aliwahoji wanawake kama Mary J. Blige, Janet Jackson na Chaka Khan.[1] Carey aliendesha vipindi hivyo vya wki katika kituo cha HLN, vilifahamika kwa jina la "What Matters," humo aliongelea masuala ambayo watu wa Marekani wenye asili ya Afrika wanakumbana nayo. Anafahamika zaidi kwa uhusika wake katika kuendesha kipindi cha ‘’Fort Hood’’ jijini Texas pamoja na wiki moja aliyokuwa nchini Bosnia ambapo alielezea kazi walizofanya Askari wa kikosi cha kwanza cha wamarekani wenye kambi yao nchini humo.[2] On July 11, 2013 she was announced as one of the first news anchors at Al Jazeera America.[3] Baada ya kufungwa kwa kipindi cha ‘’Al Jazeera America’’ mnamo Aprili 2016 akawa mtangazaji wa kipindi cha ‘’Al Jazeera English’’ huko Doha, Qatar na kuwa miongoni wa waendesha kipindi cha Aljazeera America wachache waliobakishwa. Mnamo Oktoba 2020, akawa muendesha kipindi wa muda wa ‘’UpFront’’ kilichorushwa na ‘’Al Jazeera English’’, hii ilikua ni baada ya kuondoka kwa mtangazaji Mehdi Hasan, aliendesha kipindi hicho mpaka Marc Lamont Hill alipochaguliwa kuwa muendesha kipindi hicho.

Mashirika

hariri
  • Raisi msaidizi wa Bodi ya wakurugenzi ya ‘’Men Stopping Violence’’[4]
  • Mjumbe wa bodi ya ‘’Girl Scouts of Greater Atlanta’’[1][2]
  • Tuzo za ‘’Emmy award’’-uandishi wa Habari katika kituo cha KMOV[1][2]
  • Muandishi Habari chipukizi – imetolewa na ‘’Houston Association of Black Journalists’’[2]

Uwakili

hariri

Carey ni wakili wa Watoto wakike na wanawake, akiwa amejikita zaidi katika haki za Watoto na wanawake katika masuala ya ukatili wa kijinsia.[1]

Familia

hariri

Mama yake na Carey ni mhudumu wa afya anayefanya kazi kwa kuhudumia Watoto wadogo kutoa maeneo yenye umaskini uliokithiri.[1] Anatokea katika jamii ya watu weusi.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Meet Richelle". Richelle Carey. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-03. Iliwekwa mnamo 16 Mei 2013. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "CNN Programs - Anchors/Reporters - Richelle Carey". CNN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 15, 2013. Iliwekwa mnamo 16 Mei 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Al Jazeera America Names 4 Anchors Ilihifadhiwa 26 Julai 2018 kwenye Wayback Machine. The Wrap, July 11, 2013
  4. Richelle Carey Huffington Post
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Richelle Carey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.