Richie Mensah

Mwanamuziki wa Ghana

Richie Mensah (alizaliwa 17 Mei, 1986), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii la Richie, ni mwimbaji, mtayarishaji na mtunzi wa nyimbo wa nchini Ghana.

Richie Mensah

Baada ya kutayarisha nyimbo za wasanii kadhaa, Richie alianzisha rekodi lebo ya Lynx Entertainment [1] [2] na akatoa albamu yake ya kwanza ya All of Me kwenye lebo hiyo mwaka 2008. [3] Tangu wakati huo ameshinda tuzo kadhaa kama mwimbaji na mtayarishaji wa rekodi na kudhihirisha kuwa mmoja wa watu wenye majina makubwa katika tasnia ya muziki ya nchini Ghana.

Maisha ya awali

hariri

Richie alizaliwa Accra, Ghana, na alianza kutumbuiza akiwa na umri wa miaka sita pamoja na kaka yake na dada yake katika maonyesho mbalimbali ya ndani. Aliamua kuanza taaluma ya muziki alipokuwa akisoma sayansi katika Shule ya upili ya Achimota, Accra. Richie alihitimu kutoka Shule ya Upili ya Achimota mnamo 2003 na kuanza kutoa rekodi alipokuwa akisomea uhandisi wa programu za kompyuta katika NIIT, Accra.[4][5][6]

Marejeo

hariri
  1. Aglanu Dela Ernest (17 Agosti 2009). "Richie – One of Ghana's Brightest Sound Engineers". Ghana Music. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Richie". Museke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-14. Iliwekwa mnamo 2022-04-24.
  3. Nii Atakora Mensah (25 Februari 2009). "Richie tells fans to be ready for 'All of Me'". Ghana Music. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2012. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. http://www.modernghana.com/music/15768/3/lynx-entertainment-to-launch-039back-to-zero039.html
  5. https://web.archive.org/web/20150414101443/http://www.ghanamusic.com/news/top-stories/ghana-music-awards-2010-winners/index.html
  6. http://www.modernghana.com/music/12162/3/richie-came-richie-sang-richie-conquered.html
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Richie Mensah kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.