Ronnie Mutimusekwa

Ronnie Mutimusekwa (jina la kuzaliwa: Rogers Mutimusakwa; 1955-1992) alikuwa mwanaharakati wa kwanza wa kupambana na Ukimwi nchini Zimbabwe, Afrika. Huyo raia wa Zimbabwe alikuwa mwanaharakati maarufu mwaka 1989 wakati alipoweka mambo hadharani kwamba yeye aligundulika kuwa na maambukizi ya UKIMWI. [1] Lengo lake lilikuwa ni kuvunja mwiko unaozunguka wahasirika wa VVU / UKIMWI, akitumaini kwamba utawachochea wengine kama yeye, na pia kusaidia katika juhudi za kuzuia. [2] [3] Wakati huo ilidhaniwa vibaya kwamba VVU / UKIMWI ni jambo dogo nchini Zimbabwe, lililowekwa kwa wanaume mashoga tu na wanawake makahaba. [4]

Mutimusekwa alifanya kazi bila kuchoka kukuza uelewa wa ugonjwa huo, akisimulia hadithi yake shuleni, makanisani na kwenye ukumbi. Aliunda kikundi cha kusaidia watu walioathirika na UKIMWI, kilichoitwa Ihawu (Shield) , ambacho alikuwa mwenyekiti wake ronnie. [5] Ihawu iliandaa mikutano katika viwanda ambapo wanachama walijaribu kuelimisha umma. [6] Mutimusekwa alipokea ufadhili kutoka UNESCO na Baraza la UKIMWI la Matabeleland kuanzisha ofisi huko Bulawayo ambapo alisaidia kukuza njia za kielimu za kuzuia UKIMWI katika maeneo ya vijijini, kama ukumbi wa michezo wa jamii. Hadithi ya Mutimusekwa pia ilijumuishwa katika vifaa vya kufundishia nje ya nchi. [7]Karibu watoto wote nchini Zimbabwe kwa sasa wamefundishwa kuhusu VVU na UKIMWI shuleni.

Marejeo

hariri
  1. Perlez, Jane (November 24, 1989) "Zimbabwe Resisting Facts In AIDS
  2. Edlin, John (September 30, 1990) "Most AIDS cases are in Africa; Rate likely to increase". St. Louis Post-Dispatch.
  3. Livingston, I.L. (1992). "AIDS/HIV crisis in developing countries: the need for greater understanding and innovative health promotion approaches". In: Journal of the National Medical Association, New York, Vol. 84, no. 9, p. 766.
  4. http://www.apnewsarchive.com/1990/Africans-are-Main-Victims-of-the-Global-Spread-of-AIDS/id-4416af50cc0dd0a4449d226fb496e049
  5. http://www.apnewsarchive.com/1990/Africans-are-Main-Victims-of-the-Global-Spread-of-AIDS/id-4416af50cc0dd0a4449d226fb496e049
  6. http://www.chronicle.co.zw/
  7. http://www-wds.worldbank.org/external/default/WDSContentServer/WDSP/IB/2007/02/21/000310607_20070221130319/Rendered/INDEX/386930SZ0Basic1DWPS1No110901PUBLIC1.txt