"Run DSM" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 24 Julai, 2015 kutoka kwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, P the MC akiwa na Young Killer Msodoki na Dully Sykes akiwa katika kiitikio. Wimbo umetayarishwa na Dully Sykes kupitia studio yake iliyopo Tabata, Dar es Salaam - Studio 4.12. Kiujumla wimbo unahusu majigambo ya kuiendesha Dar es Salaam kimuziki huku wengine wakisanda.

"Run DSM"
Wimbo wa P the MC akiwa na Dully Sykes na Young Killer
Umetolewa 24 Julai, 2015
Umerekodiwa 2015
Aina ya wimbo Hip hop
Lugha Kiswahili
Urefu 4:29
Studio Studio 4.12
Mtunzi P the MC
Young Killer Msodoki
Dully Sykes
Mtayarishaji Dully Sykes

Historia

hariri

Wimbo huu umetengenezwa kiajabu-ajabu sana. Awali P the MC alipigiwa simu na msanii ambaye yupo lebo ya Dully anaitwa Tony Cousin. Tony alikuwa na ngoma yake pale studio lakini hakutaka kumshirikisha msanii mwengine yeyote wa hip hop isipokuwa P the MC. Dully aling'aka kidogo, alidai huyo P the MC ndio nani, hamjui wala hajawahi kumsikia. Pamoja na ung'ako wote wa Dully, haujazaa matunda. Tony aliendelea kumng'ang'ania P arap katika wimbo wake. Hatimaye Dully anakubali na Tony kumuendea hewani P the MC.

P anaanza safari ya Tabata na ndani ya dakika kadhaa akawa keshatunga ubeti wa wimbo alioshirikishwa na Tony. Kitendo cha kutunga ubeti ule ndani ya muda mfupi kulimwacha hoi sana Dully. Dully akamgusia P ya kwamba kuna wasanii wakubwa kabisa hapa Tanzania na wana majina makubwa na unawajua - sikutajii jina lakini hawana uwezo wa kutunga ubeti kama huo ndani ya muda mfupi. Wangemaliza siku nzima.

Mbaya zaidi floo alizofanya katika wimbo zilimwacha mdomo wazi Dully na kumtaka wafanye japo dude moja ili kutimiza yale masham-sham yake. Siku ya pili wanakutana na kuanza kutengeneza mfano awali wa mdundo wao, Dully anamkabidhi fremu ya mdundo P na siku ya pili saa tano asubuhi P anamwendea hewani Dully ya kwamba keshamaliza kuchorea fremu ile hivyo tayari kwa kuingiza sauti. Dully kama kawaida yake sio mwepesi kukubali, anamchongea P huenda ukawa umeandika vitu vya ajabu, lakini baada ya kukutana, hali ilibadilika na Dully kubaki mdomo wazi.

Baada ya kumaliza kuingiza sauti, Dully ana bloo mapigo, anaanza kuwapigia simu watu kibao kuhusu ngoma hii huku akitaja jina la P the MC. Kitu cha kuchekesha, Dully alikuwa anamwona P kama msanii mpya sana, ilhali P ni wa muda, kabla ya 2015. Kila anayempigia wanamwambia Dully tunamjua huyo. Jambo hili lilimshangaza sana Dully. Inakuwaje yeye hana taarifa kuhusu P the MC. Wimbo huu alisikilizishwa kila msanii aliyekuja studio 4.12 Tabata.

Kutokana na utaratibu wa Dully aliokuwa anaufanya kuusilizisha wimbo kwa watu mbalimbali, hatimaye kaona bora hata kiitikio aimbe mwenyewe. Siku ilivyofika ya kutoa kiitikio alimaliza kazi yake. Lakini bado ikiwa kama demo katika mashine. Siku moja Young Killer Msodoki anatembelea studio, Dully kama kawaida anamsikilizisha dude lililofanywa na P, Killer anauchuna, lakini kadiri siku zinavyoenda, akili haimpi. Killer anavunja ukimya kwa kumwita chemba P, anamdokezea kuhusu juhudi aliyofanya katika dude lake, P anashukuru. Killer anatoa angalizo la kutaka kupewa taarifa siku ya kufanya video. Bila kujua P anadhani Killer anataka kuuza sura. Siku zinasogea za kufanya video, Killer anafunguka kama anataka kuwa sehemu ya wimbo. Bila kinyongo P anaupokea ujumbe wa kuwa sehemu ya ngoma. Wanarudi kwa Dully na taarifa za kushirikiana katika wimbo na Dully bila kupinga anamuongeza Killer katika wimbo.

Wimbo ulikuwa na beti 2, baada ya Killer kuongezeka, ukawa na beti 3. Wimbo unakamilika, na harakati za kufanya video zinaanza. P anafahamiana na Mims (mwongozaji wa video kutoka Fine Image - Fi). Mims anamtaka P amtumie sampuli ya wimbo ili aweze kuandikia muswaada andishi. Bila kuchelewa muswaada andishi unakabidhiwa. Wazo ni kupiga katika eneo la Matrekta, P anapanga eneo la Vingunguti Becco na kufanya sehemu ya video pale kabla kwenda kumalizia vipande vya mwisho kule Tanganyika Packers. Mims katoa ofa tu kwa P hasa kwa mahusiano yao na kutaka kumsogeza kutoka hatua moja kwenda nyengine. Tangu hapo, mawasiliano ya Mims na P yakazidi kuwa bora zaidi.

Maudhui

hariri

Ubeti wa kwanza

hariri

Ubeti wa kwanza unathibitisha kuwa uwezo wa kutunga ni kipaji, hasa ukijijua. Bila Mola kukuwezesha hakuna namna. P anachana kijeuri sana ubeti huu kwa kuonesha hao wanaojiona bora zaidi. Hakuna ambalo watalifanya ashindwe, huenda akawa zaidi yao. Rejea mistari kama vile;

"Kwa jinsi navyoizinga rap, hawapiti majamaa,
Wanashangaa kuona kila biti natambaa,
Wanajiuliza yuko vipi huyu kachaa?
Ahsante kwa mwenyezi maana niko fiti mpaka raha,
Wote ma MC viburi watakoma,
Kama rap ganja basi mpaka puli nishachoma".

Tambo za kuona kama kuna jambo umefanya na watu wanaweweseka, unataja katika mistari bila kificho. Anatoa salamu kwa waliotangulia na kuona wameishika DSM, mbaya keshaingia na uliyetangulia potea. Reejea mistari;

"Machizi wanapiga yowe "MWANA NZURI MPAKA NOMAA",
Mi ni mwendawazimu sifai katu,
Padri toka kuzimu nanywesha divai wafu,
Unayejifanya we ndo bingwa wa rap,
Haya potea, m-baya nishatinga kwa map,
Usifanye usiku nije "knock your doors",
Naked with ma di**k straight like pinocio nose,
Coz, nataka nije run DSM.

Katika kila mwisho wa ubeti anarudia mstari wa; And i dont' want to be the same"
"So lets gooo."

Kiitikio kinasema hivi;

"Eyo whatsap, haters na machizi wangu wote kwenye rap,
Mimi ndo mwenyewe na nshatimba kwenye map,
Ona nazitafuta nazo zaja chap chap...... Nataka run DSM,
Na.... nana nanana nana naa,
Nana nanana nana naa x 2

Ubeti wa pili

hariri

Killer anasema mapenzi hayana shule na bindamu hatufundishwi kupendana. Ni vitu vinavyotokea vyenyewe. Hapa alipo haikuwa rahisi kufika, bali juhudi zilifanyika. Wapo waliotaka kumuangusha, lakini kwa mapenzi yake Jalali kayashinda. Killer anahoji wezo za wachenguaji baadhi yao mistari yao hairidhishi. Waandika ilimradi tu.

Rejea mistari;

"Mapenzi hayana shule binadam hatufundishwi kupendana,
Sijahit bure muda ule haikuwa rahisi kusimama,
Haikuwa njama nlikazana kibishi,
Sio kama rap ya kweli hakuna, ila wanaochana hawaridhishi".

Killer na wasanii wanaobebwa, yeye si mmoja wao. Kipaji kimo ndio maana yupo alipo. Kuthibitisha hilo anasema muziki hauna pesa alizotarajia, lakini sio sababu ya kutoendelea kutoa dawa. Tazama mistari;

"Leo nakamua kikauzu,
Na najua kuwa hata akili inahitaji nguvu,
Ili i-move, nisonge mbele niwaache mazuzu,
Nawachenga ambao mtihani wa kubebwa wamefuzu,
Vinakera vikwazo, kipaji ndo chanzo,
Mziki hauna hela nlizotarajia kuwa nazo,
Futa mawazo, presha na aibu".

Kwa jeuri anauliza, nini maana ya muziki. Kuchana sana bila mpangilio kunapoteza mashabiki. Kuchana kunataka wasaa, tungo zieleweke kupitia vipaji tulivyonavyo na si ilimradi. Wazo ni lilelile ni kuwalaza waliotangulia kwa kuiendesha DSM. Rejea mistari;

"Nini maana ya muziki kama uwezo hautumiki,
Ukichana kupita kiasi unapoteza mashabiki,
Skia, nataka nije run DSM."

Kama alivyomalizia P, nae anamalizia na kibwagizo kilekile cha;

"And I don't want to be the same, so let's gooo".

Ubeti wa tatu

hariri

P anasema unaweza kuwa na nyimbo chungumzima lakini zote zogo tu. Hazieleweki. Tungo zake imara zilizotimia misingi. P anasema yeye ndiye sumu ya marapa, lakini ya mapenzi muulize Belle9.

"Unaweza kuwa na nyimbo tele, yah ukafanya nyingi,
Ila zote kelele zaidi ya kengele ya Misanya Bingi,
Mi nitadumu hadi milele kwa misingi,
Hadi siku navishwa suti tai mbele kama dingi,
Ukiniita "booth" haina kwere man,
Waulize wanaonijua kwenye rap niko very fine,
Tena huaga sioni gere man,
Sumu ya marapa mimi ya mapenzi muulizeni Belle 9".

Tazama pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri