Tabata ni kata katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 12103 [1]. Kata hiyo ipo jijini, katika wilaya ya Ilala, mtaa wa Mandela.

Tabata kwenye ramani

Kata ya Tabata imegawanyika katika maeneo mengi; baadhi ya hayo ni kama Tabata Bima, Tabata Kimanga, Tabata Shule, Tenge, Tabata, Segerea, Mandela na Msimbazi.

Baadae ikaja kugawanyika na kuzaliwa kata kama Kimanga, Liwiti, Segerea na Kinyerezi.

Tabata Kimanga ni eneo ambalo lina watu wengi, wakiwemo wafanyabiashara, na shule za serikali zipatazo nne ambazo ni: Kimanga, Tumaini, Kisukuru na Makoka.

Pia katika sehemu hiyo kuna kituo kikubwa kimoja (stendi ya daladala).

Marejeo hariri