Salome Joseph Mbatia
Salome Joseph Mbatia (27 Disemba 1952 – 24 Oktoba 2007) alikuwa naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nchini Tanzania.
Maisha ya Mwanzo
haririMbatia alipata elimu ya msingi katika shule ya St. Anna kuanzia mnamo mwaka 1959 mpaka 1966.
Aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya St. Joseph mnamo mwaka 1967 hadi 1970 na baadaye kidato cha tano na sita katika shule ya Wasichana ya mjini Korogwe (Tanga) mwaka 1971 hadi 1972. Alisomea shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1973 hadi 1976.
Kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alisomea Shahada ya Uzamili kuhusu Menejimenti huko nchini Marekani na baadaye akasomea Diploma ya Uzamili katika Utawala na Menejimenti huko nchini Uholanzi, hiyo ilikuwa mwaka 1993.
Shughuli za Kiserikali
haririAliteuliwa kuwa Naibu Waziri mnamo Januari ya mwaka 2006 katika Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, kabla ya kupelekwa katika Wizara ya Maendeleo ya Wanawake, Watoto na Jinsia.
Kifo Chake
haririSalome Mbatia na dereva wake walikufa baada ya gari walilokuwamo aina ya Nissan Patrol kugongana na gari lingine kubwa aina ya Fuso lililokuwa limebeba mbao eneo la Kibena, wilayani Njombe mkoani Iringa, Tanzania.
Tazama pia
haririViungo vya Nje
hariri- Mapokezi ya mwili wa Mbatia Archived 28 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- Bunge la Tanzania