Njombe (mji)

(Elekezwa kutoka Njombe)


Njombe ni halmashauri ya mji wenye hadhi ya wilaya katika Mkoa wa Njombe nchini Tanzania yenye postikodi namba 59100 [1]. Ni pia makao makuu ya Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Njombe Vijijini. Misimbo ya posta ni 59101 (mjini, CBD) hadi 59117.

Njombe
Njombe is located in Tanzania
Njombe
Njombe

Mahali pa mji wa Njombe katika Tanzania

Majiranukta: 9°20′00″S 34°46′00″E / 9.33333°S 34.76667°E / -9.33333; 34.76667
Nchi Tanzania
Mkoa Mkoa wa Njombe
Wilaya Wilaya ya Njombe Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 130,223 katika eneo la halmashauri

Njombe iko kwenye kimo cha mita 2000 juu ya UB kwenye sehemu ya mashariki ya milima ya Kipengere, hivyo tabianchi ni baridi kiasi[2]. Mji uko takriban kilomita 200 kusini kwa Iringa na kilomita 150 upande wa kaskazini-mashariki kwa Mbeya.

Hadi mwaka 2012 kata za mji wa Njombe zilikuwa sehemu ya Wilaya ya Njombe ya awali; baadaye Njombe Mjini na Wilaya ya Njombe Vijijini zilitengwa kuwa halmashauri mbili za pekee. Kabla ya kugawiwa eneo la Njombe lilikuwa sehemu ya Mkoa wa Iringa.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ya Njombe Mjini ilikuwa na wakazi wapatao 130,223 waishio humo. [3]

Wenyeji ni hasa Wabena. Lakini pia, kuna wingi wa watu wa makabila mengine kama Wakinga na Wapangwa.

Kanisa Kuu Katoliki Njombe Mjini

.

Usafiri Edit

Barabara ya lami kutoka Makambako kwenda Songea inapita mjini. [4]

Kituo cha karibu cha treni za TAZARA kipo Makambako. Pia kuna uwanja wa ndege eneo la Chaugingi.

Hakuna huduma ya ndege za abiria.

Dini Edit

Njombe ni makao makuu ya Dayosisi ya Kusini KKKT ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na pia ya Jimbo Katoliki la Njombe ya Kanisa Katoliki Tanzania. Kuna pia makanisa mengine na misikiti.

Eneo la Yakobi katika mji wa Njombe linatunza jina la kituo cha Wamisionari Walutheri Wajerumani waliofika mnamo mwaka 1899. Wakati wa Vita ya Majimaji kituo cha Yakobi kilishambuliwa na kikosi kilichoongozwa na chifu Mbeyela.[5]

Marejeo Edit

  Kata za Wilaya ya Njombe Mjini - Tanzania  

Ihanga | Iwungilo | Kifanya | Lugenge | Luponde | Makowo | Matola | Mji Mwema | Njombe Mjini | Ramadhani | Utalingolo | Uwemba | Yakobi


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Njombe (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.