Salome Joseph Mbatia

(Elekezwa kutoka Salome Mbatia)

Salome Joseph Mbatia (27 Disemba 195224 Oktoba 2007) alikuwa naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nchini Tanzania.

Salome Joseph Mbatia

Maisha ya Mwanzo

hariri

Mbatia alipata elimu ya msingi katika shule ya St. Anna kuanzia mnamo mwaka 1959 mpaka 1966.

Aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya St. Joseph mnamo mwaka 1967 hadi 1970 na baadaye kidato cha tano na sita katika shule ya Wasichana ya mjini Korogwe (Tanga) mwaka 1971 hadi 1972. Alisomea shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1973 hadi 1976.

Kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alisomea Shahada ya Uzamili kuhusu Menejimenti huko nchini Marekani na baadaye akasomea Diploma ya Uzamili katika Utawala na Menejimenti huko nchini Uholanzi, hiyo ilikuwa mwaka 1993.

Shughuli za Kiserikali

hariri

Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri mnamo Januari ya mwaka 2006 katika Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, kabla ya kupelekwa katika Wizara ya Maendeleo ya Wanawake, Watoto na Jinsia.

Kifo Chake

hariri

Salome Mbatia na dereva wake walikufa baada ya gari walilokuwamo aina ya Nissan Patrol kugongana na gari lingine kubwa aina ya Fuso lililokuwa limebeba mbao eneo la Kibena, wilayani Njombe mkoani Iringa, Tanzania.

Tazama pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri