Sarah Baartman (pia: "Saartjie"; Camdeboo, upande wa Mashariki wa Cape, Afrika Kusini, 1789 - Paris, Ufaransa, 29 Desemba 1815). Kawaida msichana huyo alizaliwa kijijini Gamtoos, lakini aliondoka huko pamoja na familia yake miaka kadhaa baada ya kuzaliwa.

Kaburi la Sarah Baartman katika mwinuko wa Hankey pembezoni mwa bonde la mto Gamtoos, Mashariki mwa Afrika ya Kusini.

Mnamo mwaka 1810, alipelekwa Uingereza na muajiri wake, mtu mweusi huru, aliyejulikana kama Hendrik Cesars, na mwenzake mmoja William Dunlop, mganga au daktari wa Kiingereza ambaye alikuwa anafanya kazi katika Lodge ya Kitumwa ya Cape Cape slave lodge. Walipendelea kumtumia katika maonesho jukwaani huko London kwa pesa. Sara Baartman alitumika miaka minne kufanya maonesho jukwaani Uingereza na Ireland. Alipoanza kulazimishwa katika kipindi ncha mwanzoni katika jukwaa la Piccadilly aliteka umakini wa wakomeshaji wa Kiingereza, ambao waliafikiana kwamba umahiri wake ulikuwa umepungua na kwamba msichana huyo walikuwa wanamlazimisha kinyume na matakwa yake. Watu waliweza kumuona, kumgusa, na kuzishikashika sehemu zake za siri au nyeti zake kwa malipo pamoja na sehemu nyingine za mwili wake pia nazo kwa malipo.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sarah Baartman kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.