Senene
Jika la Ruspolia nitidula anayefanana na senene
Jika la Ruspolia nitidula anayefanana na senene
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa manyofu)
Nusuoda: Ensifera (Wadudu kama senene)
Familia ya juu: Tettigoioidea
Familia: Tettigoniidae (Wadudu walio na mnasaba na senene)
Nusufamilia: Conocephalinae
Jenasi: Ruspolia
Schulthess, 1898
Spishi: R. differens
(Serville, 1838)

Senene (jina la kisayansi: Ruspolia differens) ni mdudu wa familia Tettigoniidae katika oda Orthoptera. Wapo tele magharibi mwa Kenya na Tanzania, kusini mwa Uganda na kaskazini mwa Rwanda. Baada ya majira ya mvua wapevu hukongomana katika makundi ya maelfu ya wadudu.

Mara nyingi wadudu kama senene huitwa panzi, lakini senene wana vipapasio virefu sana kuliko pronoto na jike ana kiungo kama mfuo kinachofanana na kitara kinachotumika kwa kutaga mayai. Kinyume na hivyo panzi wana vipapasio vifupi na majike hawana kiungo kwa umbo la kitara.

Kama chakulaEdit

Wakati wapevu wa senene wakionekana watu huajili kuwakusanya ili kuwakaanga kama chakula. Nchini Uganda senene walikamatwa kwa desturi na wanawake na watoto. Baada ya kukaangwa chakula hiki kilitolewa kwa waume wa wanawake wale kwa malipo ya gomasi mpya (Kiganda: gauni ya kitamaduni). Ingawa wanawake walilazimishwa kufanya kazi hiyo ya kuchosha hawakuruhusiwa kula chakula hiki. Iliaminika kwamba wanawake wanaokula senene wangezaa watoto wenye kichwa cha umbo la kichwa cha senene. Siku hizi wanawake hula senene bila shida.

Nchini Tanzania chakula cha senene hupendwa sana na watu wa Bukoba, hasa kabila la Wahaya.