Shaka Samvat ni kalenda rasmi ya kitaifa nchini Uhindi inayotumiwa huko pamoja na kalenda ya Gregori.

Historia ya Kalenda hii

hariri

Kalenda ilianzishwa mwaka 1957 baada ya uhuru wa Uhindi kwa lengo la kuunda kalenda ya kitaifa inayosaidia kuunganisha nchi hii kubwa. Kalenda ilitungwa na kamati iliyochungulia zaidi ya kalenda 30 tofauti zilizowahi kutumiwa katika sehemu na tamaduni mbalimbali za Uhindini.

Ni kalenda ya jua na muundo wake unafanana na kalenda ya Kiajemi jinsi inavyotumiwa nchini Iran.

Hesabu ya miaka

hariri

Hesabu ya miaka inaanza mwaka 78 BK. Kwa hiyo mwaka 2014 katika hesabu ya Gregori unalingana na mwaka 1936–1937 wa Shaka Samvat.

Muundo wa Kalenda

hariri

Mwaka huwa na siku 365 na kugawiwa kwa miezi 12. Kila mwaka wa nne ni mwaka mrefu wa siku 366. [1] Miezi ya kwanza huwa na siku 31, mengine siku 30. Mwezi wa kwanza (Chaitra) una siku 30 ila katika mwaka mrefu siku 31.

Mwaka huanza Machi 22 wa kalenda ya Gregori ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku. [2]

Mwezi Idadi ya siku Siku ya kwanza (kuf. na Kalenda ya Gregori)
1 Chaitra 30/31 Machi 22*
2 Vaisakha 31 Aprili 21
3 Jyaistha 31 Mei 22
4 Asadha 31 Juni 22
5 Sravana 31 Julai 23
6 Bhadra 31 Agosti 23
7 Asvina 30 Septemba 23
8 Kartika 30 Oktoba 23
9 Margashirsh (Agrahayana) 30 Novemba 22
10 Pausa 30 Desemba 22
11 Magha 30 Januari 21
12 Phalguna 30 Februari 20

Marejeo

hariri
  1. Menginevyo utaratibu wa miaka mirefu unafuata Kalenda ya Gregori
  2. Isipokuwa mwaka mrefu ambako siku a kwanza ni Machi 21

Viungo vya Nje

hariri