Shane ni filamu ya mwaka wa 1953 kutoka nchini Marekani. Ipo katika mtindo wa filamu za western yenye muundo wa Technicolor kutoka kwa wasambazaji Paramount,[2][3] inafahamika sana kwa mandhari yake yaliyochezewa filamu, uhariri, uchezwaji, na mchango wake katika mtindo huu.[4] Filamu ilitayarishwa na kuongozwa na George Stevens huku muswaada andishi ikiandikwa na A. B. Guthrie, Jr.,[5] iliyotokana na riwaya ya mwaka wa 1949 yenye jina sawa ya Jack Schaefer.[6] Ushindi wake wa sinematografia umeenda kwa Loyal Griggs. Nyota wa filamu ya Shane ni Alan Ladd, Jean Arthur (katika ushiriki wake wa mwisho, na ya rangi pekee, katika kazi yake ya filamu) na Van Heflin, na uwepo wa Brandon deWilde, Jack Palance, Emile Meyer, Elisha Cook, Jr., na Ben Johnson.

Shane
Imeongozwa na George Stevens
Imetayarishwa na George Stevens
Nyota Alan Ladd
Jean Arthur
Van Heflin
Brandon deWilde
Jack Palance
Muziki na Victor Young
Imehaririwa na William Hornbeck
Tom McAdoo
Imesambazwa na Paramount Pictures
Imetolewa tar. Aprili 23, 1953 (1953-04-23)
Ina muda wa dk. Dakika 118
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu Dola milioni 3.1
Mapato yote ya filamu $20,000,000[1]

Shane iliwekwa Na. 45 katika toleo la mwaka wa 2007 la orodha ya AFI's 100 Years...100 Movies, na Na. 3 kwenye AFI's 10 Top 10 katika kundi la 'Western'.

Hadithi hariri

 
Alan Ladd na Jean Arthur

Shane (Alan Ladd), ni mpiganaji mwenye weledi wa kutumia silaha na asiyependa kuongea sana ambaye maisha yake ya wali yamezingwa na siri nzito,[4] anaelekea katika kijiji kilichopo pembezoni mwa mji katika mabonde ya mji wa Wyoming, muda fulani baada ya Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani. Wakati wa chakula cha usiku na mkulima mwenyeji wa mji huo Joe Starrett (Van Heflin) na mkewe Marian (Jean Arthur), anagundua ya kwamba vita ya vitisho inaendelea katika wakazi wa mabondeni hapo. Ingawa wanamiliki ardhi hiyo kihalali chini ya kifungu cha umiliki wa ardhi cha Homestead Acts, mmiliki katili wa ng'ombe, Rufus Ryker (Emile Meyer), amekodisha wahuni na wasaidizi wengine ili kuwasumbua wakazi wa mabondeni hapo waondoke katika eneo hilo. Starrett anampa kazi Shane, anaikubali.

Katika duka kuu la kijiji, Shane na wanakijiji wengine wanapakia vifaa vya matumizi ya nyumbani. Shane anaingia katika baa pembezoni mwa duka, ambako watu wa Ryker wanakunywa, na kuagiza soda kwa ajili ya mtoto wa Starretts, Joey (Brandon deWilde). Chris Calloway (Ben Johnson), mmoja kati ya watu wa Ryker, anamwagia whiskey kwenye shati lake Shane. "Nukia kama mwanamume!" anamtania. Shane hajaingia mtegoni humo, akaachana na utani wa watu wa Ryker. Safari iliyofuata ya kuja mjini, Shane anarudi na chupa tupu kwa ajili ya soda baa pale, ambako Calloway anamfanyia tena istizahi. Shane anaagiza vikombe viwili vya whiskey, moja anammiminia Calloway katika shati na nyingine usoni, kisha kumpa kichapo hadi chini. Wengine wakalianzisha; Shane kakomaa nao, kwa msaada wa Starrett wakawashinda. Ryker anatangaza mikwara "safari ijayo mzozo utaambatana na moshi wa risasi."

Joey kapendezewa na Shane, na bunduki yake. Shane anamwonesha namna ya kuvaa kikoba cha kutunzi bastola na mafunzo ya kupiga risasi kwa haraka, lakini Marian anaingilia kati mafunzo hayo. Bunduki, anasema, hazitokuja kuwa sehemu ya maisha ya mtoto wake. Shane anajibu bunduki ni chombo, hakina ubora wala ubaya kuliko jembe au shoka, na kinaweza kuwa kibaya au kizuri inategemea na mtu anayekitumia. Marian anajibu ya kwamba mashamba hayo yatakuwa salama bila hata bunduki ikiwa na pamoja na Shane.

Jack Wilson (Jack Palance), mpiganaji wa kutumia bunduki mwenye uzoefu wa hali ya juu anakodiwa na Ryker, kwa makusudi anamchokoza Frank "Stonewall" Torrey (Elisha Cook, Jr.), kwa maneno ya kifedhuri na hatimaye kupandisha mori na pale mkulima huyu asiye-na-uzoefu alipojaribu kuifikia bunduki yake ili amuue Jack, hakufua dafu na hatimaye Wilson kamuulia mbali mkulima huyo. Mazikoni kwa Torrey, kuna mazungumzo miongoni mwa wakazi hao kundoka katika eneo hilo na kumwachia tu Ryker na wao wende zao; lakini baada ya kitendo cha watu wa Ryker kuwasha moto nyumba ya marehemu, punde wakapata mwongozo mpya nao si mwingine bali kupigania haki yao na kuendeleza mapambano.

Ryker anamwalika Starrett mkutanoni kujadili suala la makazi katika baa—kisha kumuagiza Wilson amuue pindi tu afikapo. Calloway, amechoshwa na mwenendo wa Ryker, anamwonya Shane huko kuna kudhulumiana. Starrett anakomaa kivyovyote vile nitapamba na Wilson, na kumuomba Shane aitunze familia yake, Marian na Joey iwapo atakufa. Shane, anatambua ya kwamba Starrett sio saizi yake kwa Wilson katika suala zima la kupigana kwa kutumia bunduki..anasema lazima niende mimi badala yake. Starrett anagoma, na Shane analazimika kumzimisha. Marian mwenye mashaka tele anamwuliza Shane kwanini anafanya anawasaidia. Kwa ajili yake, mumewe na mtoto wao na watu wote wenye busara wanaoishi katika bonde hilo wanaotaka nafasi ya kuishi kwa amani.

Wakati Shane akielekea mjini, Joey anamfuata kwa miguu. Huko baa, Shane anamweleza Ryker hawezi kushinda hili, kwa sababu tu wakati umebadilika; wezi wako wa ng'ombe na wapiganaji wako wamepitwa na wakati. Halafu anamgeukia Wilson: "Nimesikia habari kama huna lolote mwongo tu," anasema. "Thibitisha," anajibu Wilson, na kutoa bastola yake. Shane kamshinda kwa kutoa bastola haraka, kisha na kumpiga Ryker vilevile, wakati anajaribu kutoa bastola yake aliyoificha. Kabla ndugu yake Ryker, Morgan, aliyejificha dalini, kumtandika risasi ya mgongoni Shane, Joey anapiga ukelele wa onyo, na Shane anamwua Morgan vilevile.

Shane anamwambia Joey nenda nyumbani kamwambie mama yake ya kwamba wakazi wameshinda, ya kwamba hakuna tena mabunduki katika bonde hilo. Wakati Joey anamsogelea, matone ya damu yanammwagikia katika mkono wake wa kushoto; mkono wa kushoto wa Shane unaonekana kuwa na jelaha huku akipanda farasi wake. Katika tukio la mwisho la pekee, Shane anaondoka mjini pale, anasogeza mbele kitako chake cha farasi, huku akipuuzia kilio cha mvurugo cha Joey cha kumtaka "Shane! rudi!"

Waigizaji hariri

Athira kwa kazi za baadaye hariri

Sehemu kama "Come Back, Shame" na "It's How You Play the Game" katika mfululizo wa TV Batman uliomwonesha adui jina lake Shame, mwigo wa shujaa Shane.[7]

Katika filamu ya mwaka wa 2017 Logan imetoa maudhui ya kina juu ya athira kutoka kwa Shane, na kurejea maneno kadha wa kadha katika majibizano ya filamu hii katika vipande kadhaa. Wakati filamu inakwisha, maneno ya kwaheri ya Shane kwa Joey yanatajwa, maneno yaleyale, katika kabuli la Logan.[8]

Marejeo hariri

  1. Box Office Information for Shane. The Numbers. Retrieved April 13, 2012.
  2. Variety film review; April 15, 1953, page 6.
  3. Harrison's Reports film review; April 18, 1953, page 63.
  4. 4.0 4.1 Andrew, Geoff. "Shane", Time Out Film Guide, Time Out Guides Ltd., London, 2006.
  5. Shane. Turner Classic Movies. Turner Broadcasting System (Time Warner). Iliwekwa mnamo September 6, 2016.
  6. Schaefer, Jack (1983). Shane (Paperback ed.). New York City: Bantam Books. ISBN 978-0553271102. 
  7. van Heerden 1998, p. 162.
  8. What was that Western Movie in Logan? Archived 14 Machi 2017 at the Wayback Machine. at geekendgladiators.com, retrieved March 13, 2017.

Vyanzo hariri


Jisomee hariri

Viungo vya Nje hariri

 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: