Sheria za soka
Sheria za soka (kwa Kiingereza: “The Law Of the Game”; kifupi: LOTG[1]) ni kanuni zilizoundwa maalumu ili kusimamia masuala yote yanayohusu mchezo wa soka.
Sheria inaelezea idadi ya wachezaji kila timu inapaswa kuwa nao, urefu wa mchezo, kipimo cha uwanja na mpira, asili na aina za faulu refa anazoweza kutoa adhabu, sheria yenye utata kuliko zote ya kuotea na sheria nyingine kadhaa. Wakati wote wa mchezo, ni jukumu la refa kufafanua na kutekeleza kwa jinsi sheria inavyoelekeza.
Katikati ya karne ya 19, kulifanyika jaribio ya kugeuza sheria kuwa za ishara zaidi. Sheria hizi zina historia ya kuanzia mwaka 1863 ambapo kifungu cha sheria kiliundwa na bodi iliyokua ikishughulikia masuala ya soka iliyoundwa mwaka huohuo kwa jina la (The Football Association|Footba). Kwa muda mrefu sheria hizo zimekua zikirekebishwa na kuanzia mwaka 1886 ziliwekwa chini ya bodi maalumu (International Football Association Board).
Ndio sheria pekee ambazo FIFA wameruhusu zitumike nan chi wanachama wake.[2] Sheria hizi zinaruhusu utofauti mdogo baina ya nchi.
Sheria za sasa za mchezo
haririSheria
haririSheria za sasa za mchezo zipo 17, kila sheria ikiwa na kanuni na maelekezo fulani:[1]
- Sheria namba 1: Uwanja wa soka
- Sheria namba 2: Mpira wa kuchezea soka
- Sheria namba 3: Wachezaji wa soka
- Sheria namba 4: Jezi
- Sheria namba 5: Refa
- Sheria namba 6: Refa wasaidizi na mafisa wengine wa mchezo
- Sheria namba 7: Urefu wa mchezo wa soka, mapumziko
- Sheria namba 8: Kuanzisha mchezo na kurudisha mpira mchezoni
- Sheria namba 9: Mpira ndani na nje ya mchezo
- Sheria namba 10: kubaini ushindi
- Sheria namba 11: Kuoteka katika soka
- Sheria namba 12: Faulu na matendo yasio ya kimichezo
- Sheria namba 13: Mapigo huru (Mapigo huru ya moja kwa moja na Mapigo huru yasiyo ya moja kwa moja)
- Sheria namba 14: Penalti
- Sheria namba 15: Urushaji mipira iliyotoka
- Sheria namba 16: Goli kiki
- Sheria namba 17: Pigo la kona
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Sheria za soka kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ 1.0 1.1 IFAB (18 Mei 2017). "Laws of the Game". theifab.com. Zurich: International Football Association Board. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "FIFA Statutes - July 2012 edition" (PDF). FIFA.com. FIFA.
Each Member of FIFA shall play Association Football in compliance with the Laws of the Game issued by IFAB. Only IFAB may lay down and alter the Laws of the Game.