Shingo ya nchi
(Elekezwa kutoka Shingo la nchi)
Shingo ya nchi (ing./gir. isthmus) ni kanda nyembamba ya nchi kavu yenye maji kila upande inayounganisha sehemu mbili kubwa zaidi ya nchi.
Mfano bora ni shingo ya nchi ya Panama inayounganisha Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini. Mifano mengine mashihuri ni shingo ya nchi ya Suez baina Afrika (Misri) na Asia halafu shingo ya nchi ya Korintho kati ya rasi ya Peloponesi na Ugiriki bara.
Mara nyingi shingo ni mahali panapofaa kwa kujenga mfereji kwa sababu hapo umbali kati ya magimba mawili ya maji ni ndogo zaidi. Kwa hiyo shingo za nchi zilizotajwa juu huwa na mifereji yao:
- Mfereji wa Panama kati ya Atlantiki na Pasifiki
- Mfereji wa Suez kati ya Mediteranea na Bahari ya Shamu (Bahari Hindi)
- Mfereji wa Korintho kati ya Bahari ya Adria na Bahari ya Aegean
Kwa namna ya kinyume shingo la nchi huligana na mlangobahari ambayo ni sehemu nyembamba ya bahari kati ya bara na kisiwa, kwa mfano mlango wa Gibraltar.