Bahari ya Adria
Bahari ya Adria au kwa kifupi "Adria" ni ghuba ya Mediteranea kati ya Rasi ya Italia na Rasi ya Balkani.
Nchi zinazopakana nayo ni Italia upande wa magharibi, halafu Slovenia, Kroatia, Bosnia na Herzegovina, Montenegro na Albania upande wa mashariki.
Adria huelekea kaskazini magharibi kutoka 40°N hadi 45° 45' N. Urefu wake ni km 770 na upana waka kwa wastani ni km 160. Sehemu nyembamba ni mlangobahari wa Otranto wenye upana wa km 85. Eneo lake ni mnamo km² 160,000.
Mwambao wa kaskazini una visiwa zaidi ya 1,300, hasa mbele ya pwani ya Kroatia.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Adria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |