IMF
(Elekezwa kutoka Shirika la Fedha Duniani)
IMF (kifupi cha International Monetary Fund) ni Shirika la Fedha la Kimataifa. Lilianzishwa mwaka 1946 kwa shabaha ya kuboresha ushirikiano katika mambo ya fedha duniani. Kuna nchi wanachama 189. Makao makuu yako Washington DC nchini Marekani.
Kazi yake ni kuangalia siasa ya fedha na benki duniani na kuifanyia utafiti. Inatoa misaada na ushauri ikitakiwa.
Si shirika halisi la Umoja wa Mataifa, lakini hushirikiana na UM. Nchi tajiri za Ulaya pamoja na Marekani zinaongoza IMF kwa sababu ni nchi zilizoweka pesa zaidi katika mfuko wake. Mwenyekiti wa IMF huwa anatoka katika nchi za Ulaya na makamu wake ni kutoka Marekani.
IMF hushirikiana kwa karibu na Benki ya Dunia.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu IMF kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |