Siku ya Kitaifa ya Ushairi (Uingereza)
Siku ya Kitaifa ya Ushairi ni kampeni inayofanyika nchini Uingereza kwa ajili ya kuutangaza ushairi, ikijumuisha maonyesho ya wazi.[1]
Siku ya kitaifa ya ushairi ilianzishwa mwaka 1994 na William Sieghart.[2] na hufanyika kila mwaka katika nchi za UK na Ireland katika Alhamisi ya kwanza ya mwezi Oktoba.[3]. Tangu izinduliwe, imekutanisha mamilioni ya watu nchi nzima wakifanya matukio mbalimbali ikiwemo kazi za kimasomo na utangazaji.
Siku ya kitaifa ya ushairi imekuwa ikiandaliwa na Charity Forward Arts Foundation, malengo yao yakiwa kusherehekea kazi bora za ushairi na kuongeza wapenzi na mashabiki. Katika siku hiyo hujumuisha utoaji wa tuzo za Forward Prizes for Poetry.[4] Siku zilivyozidi kwenda, na washirika wengi walizidi kujitokeza katika siku hiyo, ikiwemo T Arts Council England, Literature Wales, Poet in the City, Southbank Centre, The Poetry Book Society, The Poetry Society, The Scottish Poetry Library.
Mwanamfalme Charles alishiriki katika siku hiyo mwaka 2016, usomwaji wa mashairi ya Seamus Heaney, The Shipping Forecast. Yalijumuishwa pia katika mwaka wa 2015 ikiwemo shairi la Blackpool Illuminations.[5]
Siku ya ushairi kwa mwaka 2019 ilikuwa tarehe 3 Oktoba. Matukio ya usomaji na maonyesho ya jukwaani yafanyika nchini Uingereza, dhamira yake kuu ikiwa ukweli.[6]
Historia
haririSiku ya Kitaifa ya Ushairi ilianzishwa mnamo mwaka 1999 na William Sieghart ambaye alisema, "kuna mamilioni ya watu wana vipaji vya ushairi lakini ni wakati wa muda tu,watakuja kutambulika kuhusu kazi zao, wala wasiogope kuhusu kusoma tungo zao kwa sauti.Ninataka watu wasome mashairi katika mabasi wakati wakielekea makazini, katika mitaa,mashuleni na katika maeneo ya starehe."[7] Gazeti la Radio Times liliandika "Siku ya ushairi imebuniwa ili kuthibitisha kuwa ushairi upo kila mahali katika maisha ya kila mmoja ."[8]
Gazeti la Belfast Newsletter liliandika, "Siku ya ushairi kwa siku ya jana imefuta maumivu,imebadilisha ushairi kutoka katika hali ya kitamaduni ya kawaida."[9] Gazeti la The Daily Telegraph liliandika kuwa katika jiji la London katika eneo la Waterloo station, "bodi imepewa mashairi na T S Eliot na W. H. Auden|Auden."[10] gazeti la ''The Times''aliandika Chris Meade, kisha mkurugenzi wa Poetry Society alisema, "Wasomaji wamepata sehemu ya mashairi kwa ajili ya mashairi yao,unaweza ukasoma toka pande yeyote uliyopo na itakufaa zaidi kupata ujuzi katika maisha mapya."[11] na gazeti la East Anglian Daily Times/The East Anglian Daily Times liliandika, "Siku ya kitaifa ya ushairi imepata sauti kupitia beti zake katika vituo vya treni,mashuleni,katika kumbi za sinema na katika maduka makubwa".[12]
Dhamira
haririTangu mnamo mwaka 1999,Siku ya kitaifa ya ushairi imekuwa ikibadili dhamira zake kama zinavyoonekana hapo chini:
- 2019: Ukweli
- 2018: Mabadiliko
- 2017: Uhuru
- 2016: Ujumbe
- 2015: Mwangaza
- 2014: Kumbukumbu
- 2013: Maji,Maji kila mahali
- 2012: Nyota
- 2011: Michezo
- 2010: Nyumbani
- 2009: Ushujaa
- 2008: Kazi
- 2007: Ndoto
- 2006: Utambulisho
- 2005: Ndoto
- 2004: Chakula
- 2003: Uingereza
- 2002: Sherehe
- 2001: Safari
- 2000: Sauti Nzuri
- 1999: Mashairi
Tazama Pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "National Poetry Day". Education in Scotland. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-20. Iliwekwa mnamo 12 Mei 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "William Sieghart's profile on Intelligence Squared". Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ http://nationalpoetryday.co.uk/about-npd/
- ↑ "About Us". Forward Arts Foundation. Forward Arts Foundation. 1 Novemba 2013. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "National Poetry Day". nationalpoetryday.forwardartsfoundation.org. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "National Poetry Day - 3rd Oct 2019". nationalpoetryday.co.uk.
- ↑ "Stand up and read it aloud!", South Wales Echo, 6 October 1994.
- ↑ "National Poetry Day", Radio Times, 1–7 October 1994.
- ↑ "Poets put the word about", Belfast Newsletter, 7 October 1994.
- ↑ Herbert, Susannah. "It's a beti za kiwango cha hali ya juu", The Daily Telegraph, 7 October 1994.
- ↑ Alberge, Dalya. "Poetry finds a new role in the supermarket place", The Times, 6 October 1994.
- ↑ "Pupils come up with wacky words for poems", East Anglian Daily Times, 7 October 1994.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Siku ya Kitaifa ya Ushairi (Uingereza) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |